Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NATAFUTA mchumba anisaidie KUTUMIA udhaifu wake wa KUCHUMBIWA.

>> Friday, October 17, 2008

Sinauhakika na tofauti ya utamu wa MCHUMBA wa KUJITAFUTIA ulivyotofauti na MCHUMBA wakutafutiwa.

Labda uzuri wa umuitaye mchumba, ni ile tofauti isababishayo uweze kumtambulisha kirahisi kwa watu fulani kuliko mchumba hausigeli/hausiboi au lile tu limpenzi ambalo unanogewa nalo lakini nishai kuonekananalo mchana.

Swali:

  • Unafikiri kwa nini umuitaye mchumba anatambulishika kirahisi kwa WANOKO?
  • Unajua tofauti kweli ya mchumba wa kujitafutia na wakumtafuta mwenyewe?

Lakini...
Utamu wa mchumba ni akusaidiavyo kisaikolojia kwa kukutuliza kirohochako kwa kuwa KAKUKUBALIA au UMEMKUBALIA.

Mchumba huyo huyo anaweza asiwe mtamu kama alivyokuwa mpenzi tu kwa kuwa unauhakika amekukubalia na labda hata uoga wa kujamba mbele yake hauna maana sana.

Mchumba wako unaweza hata kutomuonyesha sana yale mapenzi kwa sababu ushamvika pete au ushakuwa na ushaidi kutokana na alivyokupa mpaka siri yake ya kale kaugonjwa kake ka kifafa afanyako siri kwa wengine , na ni vigumu kukugeuka kama tu ulivyomsimulia kaugonjwa kako ka herpes.

Mpenzi wako hata bila kumtambulisha kwa maneno, unaweza kustukiwa na umati kwa jinsi ulivyokuwa huru kumfuta aliponyewa kidogo na bundi , karibu kidogo na pasipoguswa na marafiki wa kawaida ambapo umepagusa kwa uhuru kama wa RAIS KIKWETE kufanya ziara nchi za nje.



DUH!

Mchumba aliyetayari kutambulishwa kwa wakwe na marafiki NI MTAMU kwa sababu kwa kawaida hapendi kufanya kosa la kuaibishwa , kitu kimfanyacho awe MKARIMU ili usije kubadili mawazo.

Kisaikolojia, mtu yeyote aliyekubali uchumba anakaudhaifu ka kwamba amekubali na kwa muda mfupi ni vigumu kukageuza kaudhaifu kwa kukataa.

Swali:
  • Mchumba ni nini?
  • Unafurahi eeh ukiitwa mchumba?
Binadamu ni kiumbe cha ajabu!
Tokea binadamu ajue kuongea anajaribu kutafutia vitu majina na kujifanya yeye anajina.
Swali:
  • Unajua ingawa unajina lako na unatafutia vitu majina lakini ukiitwa mbwa unaweza kugeuka?


Naacha basi mkuu!Unajua na waza tu hapa!:-(

Wikiendi njema na kama tutajaliwa kinamna, basi tutakutana tena hapa baada ya siku kadhaa !

Kama unanafasi mpate kidogo mgombea umakamu wa rais Marekani, SARAH PALIN


Au rudi kidogo miaka ishirini iliyopita umpate MANU DIBANGO akiwa na binti yake GEORGIA wakikumbuka wimbo uitwao Qui est fou de qui? (Chouchou), waliourekodi wakati GEORGIA akiwa na miaka 7


Unaweza pia ukajikumbusha miaka ya 1950 na JIM Reeves akikuambia FLY AWAY


Basi mkuu ngojea turudi kwa LUCKY dube atukumbushe BACK to my ROOTS!


Jumatatu basi MUNGU akipenda!
Nakutakia kwenda msalani kwema!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:36 pm  

kaka simoni umechukua likizo. kama sio basi amka kumekucha

Simon Kitururu 10:39 pm  

@Yasinta:Nililala kidogo:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP