Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MWILI KANISANI,mawazo BILA nepi ,GESTI.

>> Friday, October 31, 2008

Nakudanganya!
Nipo kimwili, kimawazo niko nipatakapo.

Nipo nipaogopako.
Nipo nijifichapo.
Sipo unionapo.

Ukiniuliza, nitakudanganya.
Nikikuambia utaumia.

Sikudanganyi!

Chuchu ni plastiki,
katika titi mantiki nyama.

Labda ni nyama
katika kifuko plastiki

Ukweli ni kwamba nipo
Ukweli ni kwamba sipo
Ukitaka wangu mwili tumia
Maumivu ya mwili nitaumia

Ukitaka moyo wangu tumia
najua akili unatumia
Mbele ya macho yako,
akili ichupini mwako.

Kunipapasa mwili vitendo vyako
Nisafirivyo kiakili si idhini yako.

Nipo unaniona.
Sipo tokea umeniona.
------------------------------------------------------------------

WIKIENDI njema!
Si upo?
Tulia na SADE akupe Sweetest TABOO

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 6:53 am  

mkuu,raha ya kusoma usielewe kwani ukitafuna sana msomaji atajua unachozungumzia pale tu aanzapo kusoma.

Simon Kitururu 5:14 pm  

@RASTA: Kunastarehe ya kuelewa lakini, kama huelewi vibaya.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP