Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KABLA hujachomoa ,SI lazima ULIINGIZA au ILIINGIA.

>> Saturday, November 01, 2008

Kuna vitu viko tu , ukichomoa labda haikuchomekwa.
Kama tu ulivyozaliwa na makengeza, haukuchagua kuzaliwa kujikuta mkristo halafu kunajisi dhambi.

Ujanja ni kuishi tu na ukweli .
Hata kama si mjanja, hali halisi ndio ukweli wenyewe hata kama hali halisi ni kwamba hupendi bamia.

Kujilaumu kwa ukweli kuwa una matege, kwaweza kukusaidia kujisikia vibaya wakati asiye na matege, ana miguu kama njiti.

Chomoa tu ukitaka.
Si iliingia?

Kujilaumu hata kama kunaundugu na kitu kibaya , labda ndio kitu kinachokusaidia kujisikia kuwa uko hai.
Kutojilaumu kwaweza kuwa kunakusaidia tu maeneo fulani katika wewe ambayo yana kaukweli kuwa hunampango na wewe ni boaring.

AU?

Jifinye basi usikie maumivu, kama huna uwezo wa kunywa sumu.
Na kama unanguvu ya kutafuta sumu uvunguni, labda unaweza bado kucheza nguti mkekani.
Ishi basi!

Swali:

  • Una uhakika uko hai kama hujui waliokufa wanajisikiaje?
  • Nani kakuambia kucheza bao sio kazi?
DUH!
Tulia na DJ FATBOY SLIM awarushe watu UFUKWENI pale Brighton

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KKMie 5:27 pm  

"Kujilaumu hata kama kunaundugu na kitu kibaya , labda ndio kitu kinacho kusaidia kujisikia kuwa uko hai.

Kutojilaumu kwaweza kuwa kuna kunasaidia tu maeneo katika wewe ambayo yana kaukweli kuwa hunampango na boaringi."

Umemaliza Si, safi sana.

Simon Kitururu 5:12 pm  

@DINAH: Asante!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP