Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STAREHE ya KULIDANGANYA limtu ULIPENDALO!

>> Friday, November 14, 2008

UKIAMINI unachoDANGANYWA , UONGO ni UKWELI, ndio maana dini zote kwa waziaminio ni za KWELI.

UKWELI na UONGO vyote ni muhimu na vinategemeana katika kusaidiana KUISHI.
Ukweli unaweza kukutia huzuni hata wakati unanyemelea KIFURAHISHACHO.

Na....
...Mara nyingi akuulizaye ili kuhakikisha kama kitu fulani ni UONGO, ameshahisi UKWELI uko wapi.

....ni UHAKIKA wa jambo ndio umsumbuao atakaye UHAKIKA, wakati maisha yataendelea hata kama hakuna uhakika kuwa ni kweli au Uongo, kama tu tutakavyo kufa ikiwa ni UKWELI au UONGO.

Mara nyingi unanyemelea upande wa furaha ya starehe hata kwa kuhuzunisha umati, kama unafurahishwa na ni STAREHE wahuzunikavyo.

Linaweza kuwa na furaha HILO limtu ulijualo ukilidanganya kuliko kuliambia ukweli kuwa linanuka mkojo mkojo KWA MBAAALI lisipotumia MANUKATO.

Atakayekujua kama ni kweli UONGO, yuko katika MZANI, anataka tu uongezee uzito ahisiko ndio ukweli wa hali halisi ili ajisikie ahueni.

Ahueni atapata zaidi kama utamuhakikishia ndivyo alivyokuwa anahisi , kuwa chupi imeingia mnato.
Swali:

  • Unafikiri ni kwa nini unataka kujua kama ni ukweli au uongo?
  • Unauhakika sio bora kutokujua Utamu wa Ukweli wa hali halisi kuwa unachojaribu hakiwezekani?

DUH!


Lakini , labda.....
  • Lidanganye tu limependeza, litajisikia vizuri dakika kadhaa zaidi katika maisha haya magumu na mafupi ya binadamu.

  • Lidanganye tu kuwa unalipenda lenyewe tu na utalipenda mpaka ufe ,wakati unajua kuwa wewe ni binadamu na NIVIGUMU KUJUA hata dakika ijayo kama utakuwa hai au utakutana na ulipendalo zaidi , ambalo utalipenda mpaka wiki ijayo.

  • Lidanganye tu, kwa sababu kisiri linahisi kuwa unalidanganya ila linapenda kusikia tu ukilisifia.

  • Lidanganye kama halitapata UHAKIKA unalidanganya maisha yawe motomoto wakati ukweli ni VUGUVUGU.
  • Lidanganye listukie likuache ili uanze upya na jingine la kulidanganya.

AU liambie Ukweli uende mbinguni na kuliacha liende motoni kwa sababu linakudanganya.


Lakini...
...UKWELI ni mzuri kwa sababu UKWELi unaweza kuwa ni UONGO.
UKWELI ni kwamba, kila siku hata kama hutamki, unadanganya kwa ukweli.

Napenda unidanganyavyo kwa PODA na mavazi mazuri nihisi WEWE mzuri zaidi kidogo, wakati mwili unashepu kama nywelenywele za puani.

Napenda unidanganyavyo kwa tabasabu wakati unahuzuni, ili kunisaidia kusahau kuwa na mimi nina huzuni!

Lakini. narudia....
....UKIAMINI unachoDANGANYWA , kinakuwa UKWELI.
Ndio maana dini zote kwa waziaminio ni za KWELI.

Swali:
  • Hivi ni kweli inawezekana LISURA lako ZURI kila siku linazidi kuwa baya kwa jinsi unavyozeeka?
  • Umefanikiwa kudanganya Leo?

LiDanganye basi uende motoni kama unafikiri stori za mbinguni ni UONGO !

Lakini....
..... ukweli na uongo labda vinaleta maumivu ya UTAMU sawa!
SEMA UKWELI tu UMCHOSHE , si angekuchoka tu hata ungemdanganya.

NAACHA MKUU!

Tupumzike Na kupata BUSARA kwa kuangalia kidogo WANAWAKE wakipigana....

Halafu labda tumpate tena SHEIK mtoto a.k.a Muslim Saeed tuone uwezekano wa kupata BUSARA , akizungumzia kuhusu ALLAH


Au tu LUPE FIASCO aendeleze katika DAYDREAMING

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP