Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTAMU wa MALAYA ,ukilipia!

>> Tuesday, November 11, 2008

Tuzungumzie UTAMU wa maembe kama kuna KA uwezekano neno MALAYA ni MATUSI!

NA labda....
...... tofauti ya utamu wa maembe na MALAYA, ni kwa sababu tunamfikiria MALAYA katika UTAMU HUU, ingawa pia anaweza akawa ananuka maembe.

UTAMU ni UTAMU, tofauti ni kasaikolojia nyuma ya apataye UTAMU katika matarajio au hata uhakika au kukosa uhakika kuwa atapata UTAMU kama autarajiavyo.

Urahisi au ugumu wa kupata UTAMU unaweza ukarekebishwa kwa fikira kuwa WEWE MLENGA UTAMU una kitu kikuwezeshacho kukusaidia kudaka UTAMU, kama vile pesa ,KAMA sio nyanya chungu.

Urahisi au ugumu wa kuwa utapata utamu, unaweza kukuza ufikiriavyo UKUBWA WA UTAMU au uhitajivyo utamu wa asali wakati hata utamu wa MAHINDI YA KUCHOMA ungetosha.

SAIKOLOJIA YA ALIPIAYE inamsaidia tu MLENGA UTAMU kumiliki matarajio kuwa anapata atakacho kwa sababu kalipia.

Lakini...
.....Kupewa bure kunautamu PIA, hata kama hupendi vya bure.

Tatizo ni.....
...... akupaye bure , anakunyima kumiliki KIBEZI cha kulaumu kama alichokupa hakina sukari.

Na....
.....Ukilipia, hushangawi kwa kulalamika; kanyama KAMBWA kenyewe kalikuwa kidogo halafu bomba la ugali.

Swali:



Inajulikana kuwa Mwanamke na DUME wote wamejaliwa baraka za kuweza kuwa MALAYA kwa tafsiri fulani ya KAJINA HAKA katamu 'MALAYA' ,kama anapokea fedha au nanihii, kama malipo ya kitendo.

Fedha inasingiziwa kuwa ndio malipo MALAYA apokeayo YEYE kwa kutoa baraka KWAKO kwa kujishughulisha ili WEWE ufike safarini au AKUPE nafasi kwako WEWE uonyeshe maringo yako KATIKA SHUGHULI ili ufike , IKIBIDI ,bila hata kufikiria asikiavyo utamu YEYE .

Lakini...
... MALIPO ni malipo hata kama sio fedha utumiayo katika biashara yako ya UJIMA, ndani ya nipe nikupe, ambayo ukinipa chumvi nitakupa muhogo.

Na labda unalipa kwa kumfundisha hesabu na wala sio kwa kumnunulia chipsi dume wakati wa mapumziko.



Swali:
  • Si inasemekana hakuna cha bure?
  • Si wewe mkali wa masomo halafu unaboa na hukawii kufundisha MTU ukichekewa?
  • Hivi mahari sio kulipia?

Labda ni kweli kufurahia kwako ulichotumia kulipia, hata kama ni senene, ni kwamba ulitaka kulipia na alitaka kulipwa .Na utaondoka kiwanjani ukijitutumua kama jemadari kwa sababu umelipia ,na yeye ataondoka anacheka mwenyewe kama HAKENUI MENO, kwa sababu kakulipisha zaidi kidogo bila kusafisha vizuri sehemusehemu za haja ndogo.


Sasaaa...
.....inawezekana labda unalipia UTAMU kwa lijamaa lako ingawa umelioa, limekuoa au ni LIJAMAA ambalo UNALIFIKIRIA tu kwa sasa, na hata siku moja hutawahi kujadili bei ya KUWA limtumwa lake kwa kisingizio wanadai maisha ya uhusiano ni magumu, MVUMINILIANAGE tu, kwani hata MAUMIVU ni UTAMU.

Unaweza usistukie ...
......kisaikolojia, hulipii kama hufikiri ununuavyo ni kununua au kumnunulia .

Lakini...
.....kama unapenda vya bure, utapenda tu vya bure UKIPATA.
......ukipenda vya kulipia , LIPIA, labda ndio furaha yako HATA KAMA bure unaweza kupata .

Kwa sababu labda vya bure , unahisi ni bure kwa sababu HATA ULICHOLIPIA kitakuwa bure mpaka uhisi UNALIPIA.

Kama unafaidi zaidi nanihii ukilipia, lipia ufaidi ,kwa sababu labda unalipia hata kwa kujiuliza sijui ulipie au la.Kwa maana vya bure upatavyo HATA KAMA NI VITAMU , utahisi haviji na kachumbari kwa juisi ya ukwaju, kitu kitakacho kuhakikishia mapungufu TAMU TAMU ya UTAMU.
Swali:
  • Unahisi hujawahi kulipia utamu?
  • Hivi ukitenda mazuri ,wanaodai utalipwa mbinguni ,unafikiri wanazungumzia malipo gani kama hujawahi kulipia hata kupiga chabo , kama shoo yenyewe bei ghali?

NAACHA MKUU!
Ngojea Sheikh YUSUF ESTES abadilishe topik na kuongelea kama unaruhusiwa kuangalia TV

Au ngojea MWANAFALSAFA aeleze asitavyo KUOA katika BADO NIPONIPO:

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KKMie 9:39 pm  

Aisee! Sasa saikolojia ya wale wachuna mabuzi ndio ikoje?

Simon Kitururu 6:29 am  

@DI: saikolojia ya mchunabuzi ni faraja ya kupata kwa kuchuna akilengacho wakati anachunika maeneo.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP