Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA ukweli kuhusu WEWE na MIMI uko KWENYE SIRI!

>> Thursday, November 27, 2008

Siri ya MCHOYO ajulikanaye kwa UGAWAJI, labda iko kwenye kasiriafichako, kuwa anagawa kwa shingo upande ingawa anatabasamu, na ingewezekana ,angejifaidi mwenyewe kwa jinsi ajipendavyo.

Siri yako na mimi yaweza kuwa ndio ukweli kuhusu wewe na mimi.

Siri zawezakuwa siri kwa mwenye siri, ndio maana anaaina fulani za siri.

Hatujui!
... labda DUME ZIMA linatamani wanaume wenziye ingawa linajulikana kwa kumpa mimba mama mdogo baada ya kufanikisha kwa MADAI ya bahati mbaya kumpa UJAUZITO hausigeli .

Hatujui!
....labda sista du anaUUME ingawa gauni na ushungi vya MPENDEZA na vyamtiahamu ya UKE ustadhi.

Hatujui!

......labda wanasiasa tuhisio tunajua waongo, ndio wakweli kuliko wahubirio dini WAKWELI kwa kujifanya wakweli kwa jambo wasilo na uhakika watuhakikishiavyo UHAKIKA.

HATUJUI labda!

  • SI ni SIRI?

NAACHA!

Ngojea BOB MARLEY avute BANGI kitu ambacho labda ni SIRI.....(usiangalie kama utakwazika)


Au twende kusikiliza shuhuda za MWANADADA aliyekuwa na tatizo la kutopatishwa Mimba na mumewe katika MCHEZO wa baba na mama, kapata MTOTO baada ya kuhubiriwa na DR Getrude Rwakatare kitu ambacho labda sio siri.....



Au twende tu SOUTH AFRIKA , Mahlathini & The Mahotella Queens wakiri ndio waanzilishi wa staili ya MBAQANGA , kitu ambacho si siri....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 6:16 pm  

Lakini lie jani nalo linakupa kiwewe vipi unaona linakupa mapepe au ni bora kuliko mahubiri ya kipepe? lakini bora jani lile kuliko uchafu wa chupi

Simon Kitururu 2:06 am  

@Markus:DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP