Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Lione, JEUSIIIIIIIIIIII ,halafu ZURI KAMA MKAA!

>> Monday, November 10, 2008

Uzuri wa kamasi lako jeupe, labda ni tafsiri tu ya Uzuri AKILINI mwako na hata lingekuwa jeusi, usingekawia KUKATAA kuanza kulilamba hadharani.

Labda rangi ya ngozi yako ni muhimu tu kama rangi ya manyoya ya TAUSI dume kumeremeta katika jitihada za kujishebedua mbele ya tausi jike atakalo kumimbisha mayayi yake.

Labda ni kweli rangi yako ikiwa tofauti kidogo na ulivyo leo , utajiona mzuri zaidi kutokana na kulizoea li rangi la ngozi yako tokea uzaliwe, ambalo halikawii kuota ukurutu kama wewe si mahiri wa kuoga.

Lakini.....
...labda binadamu anaakili kuliko kuku ingawa , kuku mweusi na mwekundu wana kawaida ya kuendeleza ushoga bila kumteta kuku wakijivu kwa kutagishwa na JOGOO lenye rangi ya kahawia kwa mbaaaaali!

Swali:

  • Hivi ni kweli ZERUZERU hana rangi halafu kwa binadamu mwenye akili ,Mzungu na KAratasi vyote vyaweza kuwa vyeupe?
  • Umestukia weusi wajichubuao kama wewe ni mweusi unaweza kuwagundua zaidi kuliko weupe watumiao kila njia kupunguza weupe?

Sasaaa...

....Uzuri wa mkaa utaujua zaidi ukihitaji mkaa.

.....Uzuri wa rangi nyingine isiyofanana na rangi yako, labda unaujua kwa sababu unahitaji rangi nyingine.

TATIZO ni ....
.....NI KWELI UNAHITAJI rangi nyingine?

Uzuri wako labda unategemea umezungukwa na wabaya wanamna gani.
Na jinsi ujuavyo uzuri, ni matokeo ya jinsi ulivyojifunza na kufunzwa nini ni uzuri.

Na labda wewe ni mzuri !SIKUBISHII!
Swali:
  • Si toto baya ni zuri kwa mama yake?
  • Ushawahi kusikia mama kalinyima nyonyo toto kwa sababu ya jinsi lilivyo baya?

Jichubue, inamaana unataka kuwa mweupe kwa sababu za kujifunza kuwa utafaidi zaidi ukiwa mweupe.
Jichubue , utapendeza kama MICHAEL JACKSON.UTAJISIKIA vizuri tu kama ndio nia yako.


Hebu tumchungulie kidogo MICHAEL ,katika safari yake ya rangi...


Tatizo ni....

.....Hata uwe na rangi gani , kuna watakao iona haifai katika shughuli.
.....Ukimuuliza Barrack OBAMA , anaweza akakusimulia wampendao kwa rangi yake ,na wasio stukia rangi yake kama ilivyo kwako ingawa unafikiri kila mtu anajua KUWA wewe ni CHEUPE DAWA.

Kumbuka....
....Kuna sehemu wewe ndio haswa kivutio, na wengine wanataka kuwa kama wewe na wakiweza watajiotesha chunusi kama wewe kwa sababu umesababisha watu waone ni bomba la kitu kubinya chunusi kisimani.

.....hata kama wewe ni mweupe ushindaye juani kupata SUN TAN uwe mweusi kiduchu, bado sio mzuri kwa watu fulani halafu ni wengi tu.

NDIO....
... kwa watu fulani lazima wewe unasura mbaya ingawa wewe ni mzuri kijijini kwenu ambako ni AKILINI MWAKO.


Cha kusikitisha ni....
  • JAMANI mpaka karne hii watu waue wenzao kisa rangi tu?
  • Ni lazima Tanzania pamoja na umaskini tuanzishe biashara za kuua zeruzeru kwa nia ya kutajirika?

Mimi ni mweusi na sina tatizo na weusi wangu na labda wewe ni mweupe .
LAKINI labda kama dunia nzima tungekuwa tunafanana na ni rangi moja, nahisi kuna kitu ingepungukiwa ingawa labda tatizo lingeendelea kisa saizi ya ULIMI WAKO MKUBWA KIDOGO KWA SHUGHULI ya kulamba na UNAUMIZA.

Katika kutafuta kujielewa sisi kama binadamu, tunatafuta sababu kibao zisababishazo tuanze kufikiria tofauti zako na zangu na sio yaliyo mengi ambayo ni ushuhuda wote ni binadamu na tunahitajiana na tuko sawa INGAWA sio SAWASAWA .

Labda lakini tofauti ni kwamba wewe una akili na mimi ni mjinga, ingawa tofauti hizo zinaweza kukupa moyo wa kuishi ili unifundishe na kuniondoa ujinga na sio kunichukia kwa ujinga wangu.

Labda wewe unanguvu mimi dhaifu.
Nitetee basi !

Wakati tunazungumzia rangi au hata uzuri , labda kuna swala la muhimu zaidi tunaloliruka lisababishalo nakuona wewe CHEUPE dawa.
Tulifikirie basi kabla hatujachukua hatua!

Lione vile, meno mabaya halafu wala sio kibogoyo, ingawa halipendi meno yake kwa KUWA limesahau kuna vibogoyo!
LooH!

NAACHA BASI!
Tupate basi hekima ya Shekh AHMED DEEDAT atukumbushe kuwakumbusha wanawake wafunike vichwa au kunyoa nywele ili USIWATAMANI...(kazi kwako kama wewe kipofu na huhitaji kuona ili uvutiwe!:-()

Au ngoja tu PADRE na SISTER watuonyeshe UPENDO.....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:52 pm  

lione zuriii halafu lina tabia mbaya, lione linavyojishebedua..... mmmm mistari ya kaka simon ni utamu sana yaana napata fikra,falsafa je mpaka tuanze kuitana wahovyo na kujichubua mbona jamaa hawajichubui hivyo siye weusi kulikoni? aa mambo matamu na raha ya kublogu jamani ndiyo hii

Simon Kitururu 8:49 pm  

@Markus:Kazi ipo!Asante Brother kwa kunitembelea hapa mara kwa mara.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP