Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MVUMILIVU anasikia MAUMIVU hata KAMA ni ya utamu kuzidi ZAIDI kidogo KAUTAMU katamu!

>> Wednesday, November 19, 2008

Mvumilivu anavumilia tu kwa shingo upande.

Ingekuwa amri yake asingetaka kujishebedua aingie katika shughuli nzima ya kuvumilia hata kama ni kuvumilia jamaa litoke CHOONI.

Kama unavumilia , imezidi KIPIMO!
Kama unafurahia kuvumilia, hauna cha kuvumilia ,UNAISHI tu na ufikiriacho kutobadili.
Utamu ukizidi , labda sio utamu ,na kunawatakao kushauri uongezee maji.

AU..
......Utamu ukizidi, labda bado ni UTAMU , kwa sababu hata CHUNGU ni aina MOJAWAPO ya utamu.
Ukiuzoea utamu uliozidi , utataka kuongezea sukari kwenye utamu wa kawaida wa jana ili izidi utamu na uwe UTAMU UMEZIDI kama ulivyozoea leo.

Tatizo ni......
...... apendaye chai ya asali anaweza kukiri maji ya kunywa ni matamu pia.

Inawezekana kabisa kwamba unasikia maumivu kama ulivyojianda kusikia maumivu, la sivyo adhabu inaweza kuwa ni mazoezi ya KICHURACHURA kama sio ya KUKONYEZA kama adhabu upewayo umejiandaanayo kwa kuwa inaitwa MAZOEZI.

NA...
.....labda mvumilivu hodari ameshageuza maumivu kuwa ndio hali halisi ya maisha yenyewe.
.....Kwa kawaida unaanza kujiandaa kuvumilia kabla chamoto hujakiona , kama tu ujiandaavyo ujuapo utakanyaga moto kama unahisi unajua maumivu ya moto .

Swali:

  • Ushajiona unavyobadilika sura wakati unajiandaa kushika moto?


Maumivu ni changamoto zaidi mwanzoni , kuliko mwishoni ukijiandaa kufa ,kama sio kukata tamaa KUWA pamoja na kuwa na roho nzuri jamii inafikiri mchango wako ni wa kifala.


Vumilia!
Inasemekana Mvumilivu hula mbivu kama sio HUZOEA maumivu.

ILA....
...wakati unavumilia, kumbuka unaweza kuzoea maumivu kama sio kufa KWA MAUMIVU.

Na uvumilivu wa maumivu ni wa maana tu kama unaleta maana kwako.
Kama unavumilia ili jamii isifie , unaweza ukavumilia halafu USILE MBIVU.

NA....
......Pamoja na maumivu yako,jamii itaendelea tu bila wewe na uvumilivu wako.
,
Swali:
  • Unauhakika kuwa huwajui waliovumili na kutokula mbivu?
Kuna ambao hawatakuambia kuwa, labda pamoja na umuhimu wa mchango wako, utachangia zaidi ukifa na kuwaachia wengine maumivu ili wajifunze kuvumilia.
UVUMILIVU nishai ndio maana unaweza kujikuta unavumilia mpaka UONGOZI wa WAHESHIMIWA wajinga katika SIASA zetu za kutafuta AHUENI.

VUMILIA lakini...
.... uvumilivu wako wakutaka KUKWEPA kufanya dhambi ili uende MBINGUNI, labda ni busara INGAWA ,hujui hata kama TOGWA uzipendazo zitapatikana PARADISO kama ZIPATIKANAVYO kule JEHANAMU kwenye uasherati na mbilimbi za KONYAGI.


DUH!
ASANTE kwa kunivumilia unajua tena nawaza tu hapa!
NAACHA basi!

Hebu tujaribu kumvumilia Rais Nyerere akiongea KISWANGLISH na WASWAHILI wenzake katika kutufikishia hekima za KUKOPA....kama S. Msafiri K. wa Safirisafariyamuziki alivyomdaka.

AU ngojea tena tumvumilie MCHUNGAJI MUNISHI aonyeshe UVUMILIVU wake kwa KIKWETE....

Twende tu basi GHANA kumpata VEEDA atulize kwa Bribi Yaaye ME

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 7:25 pm  

Wajua Simon.... ukishevumilia kula mbivu kisha ukapata lishaoza ndani...utaanza tena upya? DUH!

Yasinta Ngonyani 9:11 pm  

nakubaliana na Serina yaani usijifanye mtu wa kuvulia sana tatizo lake litakuwa hilo alilolisema dada Serinaserina. kazi kweli kweli

Simon Kitururu 6:22 am  

@Serina: Itabidi tu UZOEE uvumilivu nalo kama wewe Mkristo.Kuanza upya si dhambi:-) Ila tomasatomasa angalau kujaribu kucheki kama embe lina bikira.

@Yasinta:Mvumilivu anaweza asigundue limeoza lakini!

Yasinta Ngonyani 12:02 pm  

Haya nimekuelewa Simon

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP