Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKIJIANDAA kucheka UNAWEZA usicheke MSIBANI wakati MAITI inachekesha!

>> Friday, November 14, 2008

KUNA kitu unajua , ndio maana KUNA kitu kinakuchekesha!

Lakini...
.....Cha kwanza ufanyacho ukizaliwa, ni KULIA!
Kucheka kunakuja baadaye, halafu utachekeshwa na kitu chochote afanyacho akudongolosaye, na utacheka mpaka ukumbuke chuchu au uanze kulia kisa unausingizi, umejinyea, kama sio kujikojolea wewe toto changa.

Unaweza ukabisha!
KITU chochote ukionacho hapa duniani ni kichekesho !
Inawezekana kabisa mwendo wa BATA kwako si kichekesho lakini wamvunja mbavu mtu fulani.
NI kweli unajifunza kuchekeshwa KITU kama vile ujifunzavyo kuchamba baada ya haja kubwa.

Haki ya MIUNGU au KIBUYU tena!;...usipojua kitu, hakuna KICHEKESHACHO.


Ndio maana...
.....Watanzania wachekeshwao na ZE COMEDY wanaweza kuonekana taahira, kwa wasioelewa hali halisi ya Tanzania isababishayo hata lafudhi ya KISUKUMA imchekeshe MSUKUMA aliyezaliwa KIBAHA.

Na...
... kama EDDIE MURPHY au DAVE CHAPELLE wanakuchekesha, usishangae kukutana na adhalilikaye kwa kukushuhudia huchekeshwi na visa vya PWAGU na PWAGUZI, kama sio KIPEPE.

Usiwe na wasiwasi lakini...
...ni kweli tukikutazama unaonekana mjinga kama mimi, kwa kucheka uchekeshwapo mbele ya waiostukia unacheka nini na kwanini akijamba inachekesha.

...ni kweli mara nyingine ukianza kucheka kwa sababu kwako kinachekesha, wengine wanaanza kukucheka wewe kama tu ambao huchekeshwa na kicheko chako kiwakumbushacho kuku akipaliwa.


Swali:

  • Ushaliangalia kwa makini kubwa zima likijaribu kumchekesha mtoto mchanga?
  • Unakumbuka lugha watu wazima watumiazo kulichekesha toto changa ziletavyo maana?
Lakini....
....Inaudhi kuangalia kipindi cha vichekesho halafu huchekeshwi:-(
..unaweza kumhurumia pia ajitahidiye kuchekesha halafu hachekeshi!

NDIO...
....Wakati unahitaji kucheka , utachekelea ujinga tu hata kama unajifanya wewe hupendi mambo ya kijinga.

NA....
......labda, maisha yako yana maumivu ,kama kubwa zima unafanya maandalizi ya kwenda kuchekeshwa au unalipia ili uchekeshwe.
Swali:
  • Unakumbuka enzi zako za kucheka kwa sababu kuna kichekesho na sio KUCHEKA kwa kuwa umejiandaa kucheka kwa sababu kuna kipindi au LIMTU lichekeshalo ?


INAWEZEKANA wachekeshaji ndio watu wenye huzuni kama wewe mwenye huzuni!

INAWEZEKANA wewe na mimi ndio wachekeshaji na ndio VICHEKESHO!

Cha ajabu....
......labda unafuraha ,na labda bado unataka kuendelea kuchekelea sana kwa kujidai kumkataza akuambiaye ujinga kuwa; atakuvunja mbavu kwa kukuchekesha asipoacha kukushikashika kwa kauli tofauti na zikulizazo, kama sio kwa vidole vigusavyo kwenye kitekenyeo.

Halafu ...
.....utadhani kwenye huzuni ni vizuri kujaribu kucheka.
Cha ajabu ....
....kwenye huzuni , mara nyingine ndiko huruhusiwi kucheka , kisa lijamaa walipendalo na labda hata hukulipenda, limekufa!:-(

Kumbuka maisha yako ni yako peke yako na yanakupa uwezo wakustukia kichekeshacho kivyako mwenyewe, ingawa unachekelea KANYAU!

Siku uchekayo sana , unaweza kusahau , labda ndio siku yako ya huzuni .

CHEKELEA tu hata UJINGA, lione vile!
Nani kakuhakikishia vya maana sio UJINGA?

Chekelea tu kama unaweza na kumbuka HUZUNI inakusubiri tu kwenye KONA!
DUH!
:-(

Swali:
  • SI unakumbuka kuna walioshangilia SADAM HUSSEIN kakata roho?
NAACHA MKUU, topiki imenishinda!

Hebu twende kidogo kushuhudia jamaa likimpiga MKE wake kisiri kwenye DANSI


AU twende tu bungeni KENYA kushuhudia WAHESHIMIWA wakipigana....

AU ngojea tu niwaachie GROUNDATION wajaribu kuongea WAKATI pia UKIANGALIA PICHA za mpiganaji MANDELA

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KKMie 9:24 pm  

Hahahaha hapa ni mahali pekee hunipunguzia hasira za siasa za bongo.

Kazi nzuro Si,asante.

Simon Kitururu 6:26 am  

@DI: Asante DI!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP