Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA HUNIPENDI, nipe tu MWILI WAKO kibahati mbaya ,kwa KUTUMIA AKILI!

>> Friday, November 07, 2008

Sina makuu!
Akili zako chuo kikuu, zangu shule ya vidudu na kuukuu.

Huhitaji kumuuliza mwalimu mkuu,
dhambi waniingiza kichwani , katikati na hata kwenye miguu.

Binadamu mwana haramu weye !

Nikikuangalia , ni mtu na wala sio mwewe.
Nikiwa dhaifu, wan'tia kiwewe.
Akili natumia mpaka kudoea lako pendo weye.

Nipe mwili, roho na moyo vya Mungu wako weye.
Nipe kidogo tu , sana nitachoka, nakumtamani yeye.
Usinifunze sana, nikijua , nitataka mahiri kuliko wewe.

Nipe kidogo nichangamshe damu.
Wewe na mimi ni binadamu.
Ya roho siyajui na hayatoki damu.
Tutayajua tukifa au kuishiwa damu.

Mwenzio na hamu!
Mwili wako kuliko akili ,wan'tia hamu.
Akili zako, ujauzito hazipati, hazin'tii hamu.

Unaakili utafikiri si binadamu!

Kama hunipendi ,mwili nipe, umen'tia hamu.
Kama dhambi, mijeledi wanichapa, jehanamu.
Naomba kidogo basi weye mwanaharamu!
-------------------------------------------------------------------------------------------

Wikiendi njema!
Tutaonana Majaliwa ,na usiniulize la hapo juu, mwenzio sina hamu......

Tutembelee kidogo koo lako lakini ..............Kuangalia VOCAL CORDS zako karibu na KIDAKA TONGE




Au Koffi Olomide na Lokua KANZA waendeleze simulizi za DIABOLOS

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:57 pm  

napenda jinsi unavyoandika. majaliwa nawe

Simon Kitururu 2:08 am  

Asante Yasinta!Ujaliwe zaidi Mwanadada!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP