Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NIKIKUONA tu hata kama sijachungulia , NAANZA kupata DHAMBI!

>> Thursday, November 27, 2008

Kuna watu au hata maiti , wasio kufikirisha ya heri na baraka kama MASWALA ya MSIKITINI, KANISANI au afundishayo kungwi yakukwepeshavyo dhambi.

Labda ukiinama Msikitini au kupiga magoti kanisani unamkwaza kama tu akwazishwavyo kwa sauti yako nyororo yenye kibezi baada ya KUBANJA.

Binadamu ni kielelezo tu kama SANAMU!

Sanamu laweza kukumbusha Bikira MARIA kama tu likukumbushavyo Mwalimu Nyerere.
Muonekano wako unaamsha fikira za binadamu mwingine kinamna.

Lisichana ulipendalo inaweza ikawa ni kwa sababu linakukumbusha mama yako na LIVULANA ulichukialo linaweza likawa lina kukumbusha lijamaa ulilowahikulipenda mpaka juzi, lililofanikiwa kukusaidia kukuumiza roho kwa kukunyima NANIHII!

Swali:

  • Hivi ukiangalia picha za MAPIRAMIDI ya MISRI ,yanakukumbusha kuwa ni MAKABURI?
  • Wakati unajiangalia kwenye kioo unakumbuka unafanana na binadamu?

Lione, zuuri halafu kulitamani DHAMBI!:-(

Unaweza kuwakumbusha watu kibaka fulani mtaani ,na ukitokea ,kila mwanamtaa anaanza kuchunga pochi au chupi yake.

Kwa uwakumbushao malaika kwa muonekana na vitendo, labda kuna uwaingizao dhambi ya kujichukia kwa kuwafanya wajihisi hawafai ,kitu kiwasaidiacho kuwa karibu na malaika.

Utabakwa shauri zako!
  • Si muonekano wako unawatia watu hamu ya kidude ulichonacho kibakwacho?

Utapigwa shauri yako!
  • Si unawakumbusha watu mchawi fulani alogaye kuku?

Lakini....
...labda si kosa lako watutia dhambi kwa kuwa binadamu.

JAribu tu kuwa kielelezo chema kama binadamu.

Binadamu weye hata ufanyeje, kuna umtiaye dhambini tu.
LAbda tubu kama ni kosa lako nimechungulia na umenitia dhambi.:-(


TOPIKI IMENISHINDA!

Nawaachia Black Uhuru wazungumzie MSICHANA mwenye MACHO ya KUMEREMETA na TABASAMU la PLASTIKI katika SHINE EYE GAL/Plastic SMILE....

Au tu KRS ONE azungumzie RAFIKI katika A FRIEND

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:07 pm  

Mkuu hapo kwisha kabisaaaa. Lione zurii halafu kulitamani dhambi, wakati linajua linanitamainisha na kupata dhambi, lenyewe linaua kwamba dhambi ni mpaka ukatubu. Linajua kwamba ninapolitamani ninajisikia kujua ya sirini, pengine halina siri ndiyo maana linanitaka nipate dhambi.
LAKINI pembeni kuna jamaa halina habri naye, lakini lenyewe lipo tu kwangu. umewahi kuliona linaotokomea mitaani? lione lina dhambi kunizidi mimi lakini linajua linaniongezea dfhambi. UNAONA SASA tayari nimetenda dhambi, lakini linajua kama linanitendesha dhambi, nikimwambia ang'ata vidole na kusema maneno machache tu NDIYO, WAPI SASA. haoyo ni maneno yake kila siku, linanipa shubiri wakati linajua sistahimili? ebooo ngoja leo niliambukize dhambi maana nimechoka kutubu
ALAAA kumbe dhambi ni hisia tu, kumbe dhambi inawatengenezaji. oooohhhh
MKUU imenishinda kwaheri kwa leo

Simon Kitururu 7:21 pm  

@Markus: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP