Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Swala la MTOTO mzuri chupi CHAFU!:-(

>> Friday, November 21, 2008

Ya muhimu yako mangapi,
...kama huoni hatua ulizopiga ZI ngapi?

Kwa asiye hata na chupi,
.. ni hatua chafu chupi ,kama hana nepi.

Fahari ni ya mwenye chupi,
..ukisahau umuhimu wa tumizi la nepi.

Usafi wa hiyo nepi,
..ni mpaka uwe na nepi


Kama unahesabu ngapi,
..aliye na moja ni mwanzo wa kuwa na ngapi.

Mali iliyo makapi,
..ni mali ingawa kwako hailipi.

Mtoto mzuri kama pipi,
..nguo chupi ,maganda ya pipi.

Hata iwe nzuri vipi,
..mwisho hutupwa kama makapi.

Wamcheka chupi chafu,
..wasahau angalau ana chupi?
----------------------------------------------------------------------------------

Labda tuone zaidi kidogo ya tuonacho wakati tumekiona kinadoa.
Si angalau kipo?

Swali:

  • Kingekuwa hakipo je?
WIKIENDI NJEMA!

Tupate kidogo JAZZ kutoka kwa mwanadada nimzimiaye Esperanza Spalding



Au tu, mwanadada Tanya St. Val aje na - Zouk Chiré - Emmènes-moi

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 6:12 pm  

Mkuu hii ni hatari chupi chafu halafu akitembelea anaringa kumbe anaringia chupi yake? alal kumbe maringo na uchafu ni vitu muhimu? kumbe ukiringa unaficha uchafu? ha ha ha ha Naacha Mkuu vipi lile jani ? kumbe uchafu unaambatana na maribgo?

Simon Kitururu 2:10 am  

@Markus:anacho ingawa kichafu.Akiosha ,kipya.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP