Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda AONGELEAYE masikini ANA NAFUU kuliko MASIKINI!

>> Sunday, November 30, 2008

Kama kuna MASIKINI aongeleaye matatizo yako, kuna uwezekano ni kweli ananafuu katika matatizo yafananayo na yako.

Inawezekana ni kweli matatizo yanaweza kuunganisha watu katika tatizo.

Labda urafiki wetu ni kwa sababu wote tuna MATATIZO ya kifafa halafu tunatembea kwa mwendo wa kudunda.

Lakini labda...
...Matatizo yakikukolea , hutakuwa na muda wakustukia matatizo ya mwingine.

Kama umeshaanza kugundua tatizo la wengine , basi kuna uwezekano tatizo lako limeanza kupungua kitu ambacho ndio tatizo!:-(

Tatizo ni.....
..... mara nyingi ni ufikirialo na jinsi ulifikirivyo ndio tatizo.

Umasikini ni tatizo, wakati kuna MAMA THERESA aliyekuwa anaamini kuwa UMASKINI ndio kitu kikusaidiacho kwenda mbinguni na si kitu cha busara kujaribu kukifuta.

Wengi tunajaribu kuondoa UMASKINI kwa sababu tunajua matatizo ya umaskini mpaka tunasahau kuwa si yote katika UMASKINI ambayo yanahitaji kupigwa vita.

Swali:

  • Ushawahi kuona maskini akiwa na furaha?
  • Ushawahi kusikia tajiri atakaye kujinyonga?
Aongeleaye tatizo lako la kunuka kikwapa wakati wewe ndiye mwenye chakula na yeye ana njaa, labda njaa haimuumi vizuri ndio maana ananusa bado kikwapa kuliko harufu ya mchicha.


Ndio....
..labda maskini hana pesa.

Lakini....
....Wewe tajiri mwenye pesa uko kamili?

Labda aongeleaye maskini anaupungufu wakutostukia umaskini wake mwenyewe hata kama ni umaskini wakudhania yeye ni TAJIRI.

Labda tunaweza kuchagua tu wapi kila mtu ni maskini kama tu wapi ni tajiri .
Isije tu ukawa unaongelea umaskini wangu ilikuepuka kuufikiria umaskini wako.


NAACHA!
SIKU NJEMA!

Ngojea Dan Dennett: aongelee Ants, terrorism, and the awesome power of meme


AU Ngojea basi tumsikilize LADY SAW aongelee tatizo la Mwanamke kuishi bila KIKOJOLEO cha kiume....(usimsikilize lakini kama kuna maneno ni matusi..)

Au tu SHABA RANKS aongelee apendavyo nanihii...(Usisikilize lakini kama unahisi inawezekana ni matusi)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP