Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SIKUELEWI , labda WANAKUELEWA.

>> Tuesday, November 11, 2008

Ajaribuye, kajaribu ingawa simuelewi.
Nisipo kuelewa, wapo watakao kuelewa hata ikiwa ni karne ijayo.

Labda unajua , hata kwa sababu umesomea ndio maana unajua.
Labda kusomea kitu ni kukiri hukujua .
Labda una vyeti kama yeye na yule lakini unajua , hata kama kujua kwako ni kwamba hujui.

Labda unaonekana hujui ndio maana unahitaji vyeti, wakati sentensi yako kwa wakusikilizao , wewe ni profesa hata kama ni wa kuuza kigenge.

Tufundishe basi tusiojua!
Labda unajua tu na hata hukuenda shule ziitwazo shule , jando, na wala hukunemwa.

Kumbuka ajuaye , bado anaweza kutojua kuwa dakika ya mwisho mjuaji hana ujuzi wa mwendo wa MOYO wake kabla haujafunga breki, kama asiyejua tu .

Siku ya mwisho unaweza kushindwa kumalizia hata kikohozi wakati TUNAJUA unajua kubanja.
Toa ujuzi angali unaweza!

Ndio ....
...Nakuzungumzia wewe Injinia, Daktari, Mganga wa kienyeji , Binti Halufani na hata weye KIJEBA na Gangwe wa kimasomaso ambaye ni mjuaji...

...Namzungumzia wewe, mimi na yule......

NAAMINI KILA MTU KUNA KITU ANAJUA AMBACHO WENGINE HATUJUI.

Fikiria mara kadhaa kabla hujafa nacho UJUACHO dakika nisiyoijua na labda DAKIKA usiyoijua kama utakunywa sumu , kujinyonga , kama sio kujaribu KUAGA DUNIA kwa kujirusha mbele ya MKOKOTENI katika dakika uliyopanga ambayo unaweza USIFE na kiuno umevunja!

DUH!

NAWAZA TU hapa MKUU!

SIKU NJEMA!

Tupate Puppetry of the vagina , labda inaeleweka na tusiojua(samahani watu fulani mtakao elewa zaidi)


Au Twende kidogo ETHIOPIA kwa TEDDY AFRO atupe simulizi za JAH

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:31 pm  

aise Simoni hapo kazi ipo. mwe kazi kweli kweli:)

Simon Kitururu 8:47 pm  

@Yasinta:Si utani dada yangu!:-(

MARKUS MPANGALA 5:55 pm  

liache nilidanganye lenyewe linapenda kudanganywa wakati mimi nataka kulimenya tu. Utaona kila siku linaniuliza vipi nimependeza au? na kwakuwa nataka kula binzari bila mboga niache nilambe tu asali halafu nipate kifua kikuuu, kwani nitakufa? muone kila akisema nimevaaje namwambia umevaa vizuri halafu hicho kiuno mmmm!!! si linapenda kudanganywa, acha nilipe ujiko halafu nipate mishiko na kujinyakulia kibindoni. Naacha basi lakini siyo siri MAWZONI ni FALASAFA, yaani kazi kweli kweli

Simon Kitururu 6:30 am  

@Markus: Asante kwa kunipa tafu hapa MKUU!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP