Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Bwana au Mke wa MTU!

>> Sunday, November 30, 2008

Huna mtu wewe kama tu labda wewe mwenyewe huna wewe.
Uhusiano wako na ulichonacho ni wakujijengea mwenyewe mawazoni , ndio maana mpaka wazazi wako ni wako mpaka uambiwe walikuokota ndio wanageuka kuwa ni wazazi wako tokea walivyo kuokota.


Unaweza kuvunja ndoa kwa sababu kuna mtu amekuchukulia mtu wako.
Unaweza pia kutafuta bikira ili ujihakikishie kuwa ni wewe tu mwenye kanyau ,ingawa wewe mwenyewe si bikira.

Labda...
...kuna umuhimu wa wewe kuwa na chako ingawa unaweza ukazidisha umuhimu kuliko ilivyo kuwa MUHIMU wakati wewe mwenyewe huli NYUMBANI na hutoi UVUNGU.

Swali:

  • Mtu akikuchukulia mtu wako unafikiri kachukua nini kama hakuondoka hata na maeneo yaliyowahi kufunikwa na nepi yake?
  • Unafikiri naongelea bwana au mke wa KUKU?
  • Unafikiri kwa nini kuna WATU hawana tatizo na wewe ingawa wanajua si bikira?
  • Wewe kama mke mwenza, huyo ni mme wako au wenu?


Jinsi mtu ajifikiriavyo akishasema hiki changu, ni UKICHAA kiiidogo.
Ukikutana na mtu mwenye chake, inamaana chako kwake labda si muhimu kama chake.

Kitu chake au chetu kinaweza kuachiwa kiote MAGUGU wakati chako kinanyolewa staili za MADENGE ili kivutie.

Tatizo ni....
...ujisikiavyo na ukaribu wako na kitu chako leo asubuhi si sawa na juzi.

Kuna wakati unajua kabisa kuwa hujisikii kwamba kuna umuhimu kitu chako kiwe chako.
Swali:
  • Si, gari ulipendalo unaweza ukaliuza baadaye?
  • Ndugu yako si ni ndugu yao ndugu zako?


Kitu chetu ni kizuri wakati mwingine kama kitu changu.

Tatizo...
...kitu chetu inamaana kuna wengine pia wanatumia hicho kidude.

Si tatizo lakini kama unakiita kitu chetu wakati unajua ni wewe pekee unatumia kama wewe ni mpenda kitu changu.


Uzuri wa kuamini una chako ni kama unaweza kuhalalisha kauli hiyo kwa muda utakao kuhalalisha ni chako.





Unaweza kubisha!
Hakuna kitu chako wakati wewe mwenyewe huna wewe mara nyingi kuliko unavyoweza kukiri.
Uwezo wako wa kuwa na chako wakati hata unashindwa kuzuia chupi isiingie mnato kwako , kitu usichopenda, inawezekana uko mawazoni tu.

Kitu chako ni aina ya kujidanganya ingawa inabidi ujidanganye saa nyingine ili uhalalishe jinsi gani tokea ujue siri kuna limtu lina kuonjea, basi kinjegere au kindizi hakinogi tena kama zamani.

Kunogewa na chako kama tu kunogewa na chake iko mawazoni tu kama ubwabwa wenyewe ni uleule.


Tunza chako kwa sababu unaamini una chako.
Kumbuka.....
.....Yote yako mawazoni tu ingawa utausingizia moyo kwa kudai yako MOYONI !

Inasemekana mpaka UJAMAA ulishindwa kutokana na watu kushindwa kutunza chetu .
Inasemekana Ubepari unafanya vizuri kwa sababu unahimiza kila mtu ana chake.

Kumbuka wakati unachako kuna wasionacho kabisa na unasema unachako kwa sababu unajua kuna wasionacho kabisa.

Kuwanacho ghali!
Kama huna labda UNANAFUU!
Swali:
  • Wazazi wako si ni wako tu ingawa ni wazazi wa kaka na dada zako pia?
HAPA Nawaza tu MKUU!

Ngojea Billy PAUL alete simulizi za yeye na MKE wa MTU... katika ME and MRS JONES.


AU Dan Gilbert ajaribu kuzungumzia furaha na huzuni katika : Why are we happy? Why aren't we happy?

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:47 pm  

Simon umeniacha hoi kabisa. ila kweli kila kitu ambacho ni chako sio chako tu. Kwani hata mwili wako sio wako tu. Kazi kweli kweli.

Simon Kitururu 6:28 pm  

@Yasinta: Si utani , kai kwelikweli!

MARKUS MPANGALA 5:17 pm  

kazi kweli kweli lakini raha kweli kweli maana si unajua ukitaka cha mwenzio naye atataka chako. KWANI ukimnyima akilalamika wewe unaonaje mkuu mm hapana kuna walakini akunyime wakati TUPO KWA AJILI YA WENGINE.
looo nimechoka mkuu sijui vipi

Simon Kitururu 10:43 am  

@Markus: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP