Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna mambo yawezayo KUKUKUMBUSHA wakati UMEVAA,ni kweli CHINI YA NGUO au GWAGURO bado uko UCHI!

>> Wednesday, November 05, 2008

Wakati natafakari ushindi wa BARRACK OBAMA.............

Labda ni kweli sio sisi wote wenye ujasiri wa kufanya.
Labda ni kweli sisi sote TUNA uwezo wa kufanya.
Labda tofauti ya wafanyao na wasiofanya pamoja na mafanikio ya utengenezaji wa mimba au ugali iko nyuma ya kujiamini na kujua halihalisi au kujijua.

Waweza kujisahau na kuishi kutokana na muonekano na sio halihalisi.
Hata kama hali halisi ni ukweli kuwa wewe ni uwezaye ,waweza kujikuta unaishi kama jamii ilivyokufunza kujiona au hata baba , mama na ndugu kama sio marafiki, walivyokupiga makonzi kwa kufanya wadhaniacho hakitakiwi kufanya hata kama kinaleta firigisi mezani.

Ukifuatilia jinsi watu wapatavyo moyo na matumaini ya uwezekano wa jambo kutokana nakushuhudia awezavyo mtu mwingine, waweza kustukia kushamiri kwa kutokuwa na uhakika chini ya sura za kishujaa za watu bwelele katika kuweza jambo.


Labda kwa watu weusi tunahitaji kuhakikishiwa na Ushindi wa Barrack Obama kuwa tunaweza kutokana na halihalisi ilioshamiri duniani kuwa mtu mweusi hawezi na Obama kama mtu mweusi aliyeweza ni nguvu yetu katika kutuletea imani yetu kuhusu sisi kwetu wenyewe.

Tatizo ni kwamba .......
....matumaini kama moto wa kuni , huhitaji kuni zaidi na zaidi na wachochea moto pia ili moto uendelee kuwaka.

Halafu.......
Histori sio shule nzuri, kamatu unakumbuka kuwa, kwa watu weusi , baada ya uhuru wa nchi nyingi za kiafrika , kulikuwa na mfumuko wa matumaini kuwa tunapiga hatua kujikomboa kwa kila aina ikiwepo muonekano na sifa za mtu mweusi, kitu ambacho mpaka sasa hivi kinasumbua.

Mpaka sasa......

  • Tunaendelea kupigana Congo , na sio muda mrefu hata Kenya ambako tumaini jipya kupitia Obama linaamsha hali ya kujisifia mtu mweusi, hakukua na amani.
  • Mtu mweusi katika tamaduni nyingi duniani inaaminika ana rangi isiyofaaa.

Sasaa tukumbuke tu kuwa ...
.. ukifurahishwa sana na kitu labda cha muhimu ni kujiuliza kwanini umefurahishwa na hicho kitu.
....ukifurahia sana kuvaa nguo , jaribu kukumbuka kwa nini unavaa nguo.

Labda kuna pengo ndio maana unataka kuziba.
Kuna pengo labda ndio maana tunafarijika.
Lakini.....
...kwa nini kuna pengo ?
Swali:
  • Unafikiri kwenye pengo nilazima pazibwe?
  • Unafikiri unaweza?
TUSIUE matumaini, chochea moto.
TUSIUE matumaini, ongezea kuni moto usizimike.
TUSIUE matumaini, FANYA.
Siku njema!


Tulia lakini na Martin Luther King Jr-I have a dream


Au tulia tu na Stevie Wonder -FREE

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Christian Bwaya 7:58 pm  

Hatimaye kaweza. Penye nia pana njia. Haikuwa kazi rahisi. Kaweza bwana. Ka utani vile.

Funzo. Tusiangalie mazingira tunapotaka kufanya jambo. Tudhubutu.

Anonymous 3:20 am  

WHAT IS KENYAS GIFT TO OBAMA???

Even as we celebrate Obama’s success story, even as we with fingers closed wait for his inauguration as the 1st half black President of the USA. We need as Kenyans to ask ourselves this fundamental question. What has been our contribution to Obama Success?

His BIOLOGICAL father was a Kenyan, who however abandoned his son and escaped any responsibilities of child support. Infact Obama confesses that he learnt more form his Kenyan ‘father’ absence than from his presence. This is kenya’s EMBARASSMENT NO. 1. So his real father was the parents who took Obama in and saw him through his childhood and teenage years giving him the values that he now holds. That’s the reality Kenyans.

His ‘Cousin’ Raila has all along been a source of discredit to his good reputation. Raila with his VIOLENT NATURE, COMMUNIST ORIENTATIONS, MUSLIM ASSOCIATIONS have all been used against Obama. Infact, Raila in himself has cost Obama some support and Obama campaign team had to work hard to show how distant in thinking and association these two men are. This is Kenya’s EMBARASSMENT 2. It has not gone unnoticed to the Mc Cain campaign team that Raila call for mass protest in Kenya led to over 1500 deaths. This explains why Obama banished Raila from any visits to his campaign or why Obama campaign team has consistently turned down on 4 occassions RAILA’S MONETARY CONTRIBUTIONS totaling 40,000 USD.

Obama’s Aunt who also happen to be Kenyan has been an illegal immigrant in US for a while. This was also ANOTHER EMBARRASSMENT from yet another Kenyan.
Infact, we OWE OBAMA AN APOLOGY AS A COUNTRY. With all these bad publicity from Kenya’s heritage, Obama has been understanding enough not to talk ill of us. For that we should be grateful.

Looking on the other side, Obama’s real family in the US has been a SOURCE OF INSPIRATION AND GOOD PUBLICITY. Yet, they have been quite about it as we in Kenya tell the whole world how Kenyan Obama is.

So the reality is that KENYA HAS BEEN AN EMBARASSMENT TO OBAMA.

Simon Kitururu 5:02 pm  

@Bwaya :Kweli Kabisa!
@Anony:Very interesting !

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP