Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wajanja hawako kwenye TAARIFA YA HABARI!

>> Sunday, November 30, 2008

Kuna watu maarufu kuwa ni wajanja!
Lakini wajulikanao kuwa wajanja wanamjua mjanja hata kama si kwa jina MJANJA.

Mjanja hayuko kwenye taarifa za habari!
Mjanja hajulikani , ila walio MAKINI wanaweza kuhisi nani MJANJA.

Ajulikanaye kwa ujanja wa kutaka ajulikane mjanja, inawezekana kuna mjanja amtumiaye kuchezea watu mazingaombwe ili msimstukie nani mjanja.

Kama unataka kutatua swala, mtafute mjanja nyuma ya ajulikanaye MJANJA.
Mjanja yuko tu nyuma ya ajulikanaye na umati kuwa mjanja.

Ajulikanaye mjanja , usingejua ujanja wake bila kuwepo mjanja afanyaye MPAKA ufikirie unamjua nani mjanja, kwa sababu HUYO anasifika kwa UJANJA.

Mara kibao mjanja hajiiti mjanja na wala hajistukii au kujitambua kwa neno MJANJA ingawa yeye ndio MJANJA.

Swali:

  • Sikatika kampeni ya Obama ni Obama anajulikana kuwa ndio MJANJA?
  • SI wala rushwa na wezi waliokubuhu tuwatambuao kama WAJANJA ndio tunasikia wameshikwa?
  • Si mcheza sinema ni maarufu kuliko aliyeandika hadithi iigizwayo sinema?
Naacha basi!
Ngojea twende Haiti tukakutane na TABOU COMBO hapa akiwa na jamaa wa KASSAV katika ...
Pi Gro Pi Long


Au tuendelee tu na wa Haiti a.k.a TABOU COMBO katika "Tabou Mania"


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:19 pm  

Labda ukiwa na msiuli kama SHWAZINIGA uatkuwa mjanja, pengine ujanja unalipa zaidi ukiwa mnjanja. Pengine ujanja ni bora kuliko wajanja. Labda kweli ujanja una yake sijui

Simon Kitururu 10:44 am  

@Markus: Hata mimi sijui!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP