Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BUSARA za BINADAMU mpenda NYANI, anichukiaye kwa MADAI nina sura kama NYANI!

>> Wednesday, November 19, 2008

Moja ya kitu Waafrika weusi wafananishwachonacho na WABAGUZI wa rangi, ni NYANI.

Unaweza kumshangaa Mzungu mbaguzi apendaye nyani kukuchukia kwa kudai unafanana na NYANI mpaka ukutane na Mwafrika akutukananaye; 'NGURUWE WE!' akiripo anavyopenda NYAMA ya nguruwe ingawa anamchukia MNYAMA aitwaye nguruwe.

Watu wanakutafutia sababu ya kukuchukia kwa kutumia akili za kibinadamu ziwawezeshazo KUKUCHUKIA kama OMBAOMBA na kuwawezesha KUJISIKIA vizuri kwa sababu WAMEMSAIDIA ombaomba na swawabu kiduchu wamepata kwa MUNGU au MIUNGU wao.



Swali:

  • Hivi bado ni binadamu pekee na sio tumbili au mende uliyemsikia akisema binadamu wanaakili sana na wamebarikiwa kuliko viumbe vyote ikiwemo kuku?


Binadamu labda anaakili ndio maana anajua kubagua wazuri na wabaya.
Binadamu labda hatumii akili ndio maana anabagua wabaya kutoka kwenye wazuri.

Labda ...
...binadamu anatumia akili kubagua ingawa ikibidi atasingizia aliyenaye ;ANA ROHO NZURI halafu kwa ZIRO DISTENSI ni mzuri kuliko aonekanavyo kwa mbali na wewe UMTAZAMAYE.
Moja ya Sababu inaweza kuwa NI kujaribu kuhalalisha tu SABABU zakuwaNAYE atembeaye kwa mwendo wa kuku, baada ya kukosa wa MWENDO wa bata ampendaye mwenye sura nzuri asiyemrudishia pendo kwa kisingizio ANA sura mbaya.

Unaweza kushangaa , lakini wabaguzi ni binadamu na ingawa unaweza kuwanyoshea kidole wale BIN ADAMU wengine, mbaguzi ni wewe na mimi pamoja na yule umshangaaye kwa KUBAGUA.

Inawezekana kabisa kuwa aonaye wabaguzi hajajistukia tu kuwa kuna awabaguao yeye mwenyewe kwa visingizio......
  • mweupe sana
  • yule Mhindi
  • Huyu muarabu
  • Yule chotara
  • yeye Mgogo
  • kale kana upele kidogo
  • hili Isilamu
  • Lile Pagani
  • lile mimacho kama balbu
  • huyu..... nakadhalika sita.

Sasaa....

BInadamu ni MTUNDU!
Anawezakupenda macho yako kama ya samaki aliyekabwa na kuchukia pua yako kama kidole gumba kwa kuangalia sura yako ileile.

Uchaguzi kuwa anakupenda na kukuchukia vinaweza kusababishwa na kukuhofia au kujihofia.
Inawezekana wewe ni tishio kuwa umekuja na njaa wakati UGALI wenyewe KIDOGO ndio maana anajikuta anakuchukia kwa kumtia wasiwasi atakufa na njaa.


Nachojaribu kusema ni...
....Tukumbuke tu kuwa makini katika kulaumu watubaguao wakati hatujali tuwabaguao.

Mlalamishi sana katika UBAGUZI ,mara nyingi ni yule aathirikaye kwa kupungukiwa kitu kwa kubaguliwa.

Unaweza usijali sana kama UBAGUZI unakuongezea kakitu hasa unakokataka.

Tukumbuke kuwa kuna leo na kesho lakini

Swali:
  • Hujawahi kumchukia mtu bila kujua sababu?

Basi naacha topiki!
SI tunakumbushana tu?

Ngojea TOPIKI ibadilike OBAMA na waheshimiwa kadhaa waongelee WALIVYOVUTA Bangi....

Au kwa msaada wa S. Msafiri K. wa Safirisafariyamuziki Mwalimu Nyerere aongee tena...


Asanteni tena Wadau WOTE hasa Mliokuwanami hivi karibuni ambao wengine mtajistukia katika picha hizi zangu za karibuni....
Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

PhotobucketASANTENI sana WOTE!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP