TUNAAMBIWA leo ni siku ya UKIMWI wakati;'' WAKATI wowote ni wakati wa CHAI''!
>> Monday, December 01, 2008

Leo ni siku ya UKIMWI!
Lakini juzi na jana, kama tu kesho zina sekunde   iwezeshayo yeyote aliye HAI  kuukwaa UKIMWI au hata KUISHI na UKIMWI kabla ya kuuawa na ugonjwa kama TB ulioibuka kutokana na mwili kukosa kinga kutokana na  vichina vya UKIMWI.
Bado asilimia kubwa hatupimi UKIMWI kutokana na kuogopa kujua ukweli labda tuna UKIMWI!
Sababu kubwa ya watu kuogopa kujulikana wanao MDUDU ni WEWE na MIMI katika vitendo vyetu tuwatendeavyo WAATHIRIKA.
Kutokana na tuwatendeavyo, tufikiriayo au hata tusitishavyo mpaka matamanio  kwa tuhisiye ANAO, aliyenao  anaweza asikustue anao  ili umnyime kitumbua hata kwa ahadi angekula au kushikashika na GLOVU.
Tujikinge wakati wa kufanya NANIHII lakini!
Kikubwa zaidi...
....tujichunguze kama sio sisi tusababishao mpaka KUBWA ZIMA moja likashauri kuwe na SIKU maalumu  ya UKIMWI .
Tuchunguze tunawatendeaje tujuao wana UKIMWI  ingawa tunajifanya tuna liroho zuri lisababishalo mpaka ndugu wanashindwa kutuambia ukweli kuwa wamedaka MDUDU tena kwenye ajali ya baiskeli au toroli .
LEO NI SIKU ya UKIMWI!
Swali:
- Si wakati wowote ni wakati wa CHAI?
Hebu tusikilize mmoja wa wanaojua wanaongea nini kutokana na uzoefu....
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment