Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Busara za:LABDA jishikize TU katika ujuacho, usije ukajinyea BURE, kwa kutokujua!

>> Thursday, December 25, 2008

Kujitahidi inaruhusiwa!

Lakini...
...kuna wanaoshauri mtu ajitahidi kwa liwezekanalo.

Swali:

  • Ni nini hakiwezekani kama kila binadamu anaweza mpaka kufa?
  • Lakini unafikiri kuna aliyejitahidi kunya keki?

Labda..
...kama watu wasingefanya wasichojua , hakuna ambaye angezaliwa, halafu kungekuwa hakuna VIBATARI.

Tumezaliwa hatujui ingawa matumizi ya CHUCHU ya NYONYO yalivutia mtoto, LABDA kwa sababu tusizozijua kama tu ziendeleavyo kutushangaza kwa kuvutia wanaume MIDEVU ya MVI katika kulilia nyonyo hata wasizozijua.


Sikatai!

Ukijishikiza katika ujuacho kunauwezekano hauta haribu kwa kutokujua.

Tatizo ni....

...labda maana ya maisha ni kutaka kujua ndio maana tulizaliwa hatujui.

Na ni kweli....
....labda KATIKA kuhangaikia kujua , unaweza ukakosea kujua kuwa Mwanaidi sio Sikujua, ingawa wote ni watu na ndio maana ADUI YA MTU mkubwa, ni MTU, na kisingizio cha kwanini nimeharibu ni; SIKUJUA.

Swali:

  • Hivi si ulijifunza hata kunanihii kwa sababu hukujua?
  • AU?



Naacha!
Ngojea SHAGGY ft Rihanna na MR BEAN watusaidie kupata hekima katika ....


Au WAHESHIMIWA wazee a.k.a Senior Citizen Choir watuburudishe kwa HIP HOP....

Au nimuachie COMMON enzi hizo, amalizie katika...Take it Easy


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP