Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SIMULIZI za teremka TUKAZE!

>> Tuesday, December 23, 2008

Teremka tukaze ni kitanda ,
....ingawa chini ya godoro au mkeka hakuna SPRINGI

Tunawaelewa wajivuniao KITANDA kwa sababu ya springi,
........ingawa kitanda inajulikana si lazima kiwe na SPRINGI.

Kuna wanesao katika usafiri GIA BOKSI manyoya kwa spidi ,
........na torori lisinyemke kutokana na UKUBWA wa SPRINGI.

Kasi ya spidi si muhimu,
..hata kwa msaada wa teremka tukaze
........kama UMECHOKA-hajaCHOKA na juhudi zake za SPIDI,
..............matunda yake hayashikiki kama saa uhitajiwayoKUKIMBIA
....................hauna SPIDI.



Teremka!
Basi likikwama,
....labda MAMBO YAKO CHINI, na TARATIBU ni spidi.

Na ...
...labda ni aina tu ya utakavyo kunesa ikuamliayo ulale mkekani
........ na sio kwenye kitanda cha SPRINGI.

Swali:

  • AU?
  • Kwani unafikiri naongelea nini?

Naacha!

Ngojea mke wa John Depp a.k.a Venessa Paradis atulize kwa stori ya JOE le TAXI...


Au tu twende Holland kwa ANOUK azungumzie ya ASIYE MKE wa MTU katika NOBODY'S WIFE.....

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Egidio Ndabagoye 3:59 pm  

Kitanda cha mbao bomba :D

Mzee wa Changamoto 4:19 pm  

Labda tuanze kwa kutafsiri maana ya kitanda. Kisha tutaweza kunyambulisha kama teremka tukaze ni kitanda ama la. Kwani waweza kuita kitu gari kama kitakosa sifa za kuwa gari? Ama kumuita mtu mwanamke ama mwanamume kwa mwonekano wake wa nje tu? Mbona vingi vya nje si halisi ya vya ndani? Unanunua gari kwa kuangalia rangi? Utakuta halina injini kisha ujiulize kama haikuwa bora kunua baiskeli ambayo injini yake ni kiuno chako mwenyewe? Hivi naongelea nini? Teremka tukaze? Wacha nishuke nikishakaza ntarejea.

Simon Kitururu 12:32 pm  

@Egdio: Kwa kufanyia nini?:-)
@Mzee wa changamoto: Ndio maana tunawaita tuwadhaniao mafisadi , MAFISADI wakati labda watuonyeshao FISADI ndio MAFISADI.

Tafsiri kitu cha ajabu sana. Unaweza kutafsiri gauni kuwa ni kanzu kisa MWANAUUME kavaa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP