Inawezekana bado TUNAOMBA MPAKA shenzi MBILI na NAKADHALIKA tatu!
>> Friday, December 05, 2008
Starehe na faraja  ya waombaji , waulize waaminio Mungu.
Huachi kuomba ingawa hujapata, na kisiri una dhambi ya kuhisi pamoja na KUOMBA hutapata mpaka ufe INGAWA kwa imani UNAFARIJIKA kwa sababu  LABDA  ni MAPENZI ya MUNGU.
Labda kitufichiacho siri WAKATI TUNAOMBA, ni staili tu ya UOMBAJI!
Unaweza kuomba hata kwa kusisitizia kuwa huombi mvua zinyeshe ili kuwe na kichaka kwa sababu gesti BEI  ghali.
Labda tuna busara, ingawa tunaomba  tuepushwe na mabaya wakati  umati mzima unajua sie ndio wabaya kwa kujifanya hatuna ubaya kwa kuwa tunatoa SADAKA KANISANI na ijumaa kabla hata hatujaingia msikitini TUNAMSAIDIA MASIKINI WA PESA,  aliye tajiri wa roho , kabla ya kutema mate KIDOGO  kwa sababu OMBAOMBA ana jipu kidogo maeneo  lenye kushamiri  USAHA.
Lakini....
....Unaweza kudhani kama tungekuwa nacho labda tusingelazimika kuomba.
Labda...
....kwa sababu MBWA MMOJA hana KIDUDE cha kike na cha kiume katikati ya miguu , kwa hiyo mwenye cha kiume atalazimika kuomba agusishwe cha kike hata kama nia ni mtoto wa kiume.
Lakini bado ....
.....wenye vyote wanaomba kwa sababu hata kama kipo, kunawaonao upungufu wa chao labda kutokana na kukosa utamu wa KUOMBA kwa kuwa hakikuombwa.
Swali:
- Unajua unaweza kuwa unamuomba kwa kujifanya humuangalii?
- Unajua inawezekana ulishawahi kuomba MAZIWA kwa kulilia CHUCHU,TITI au NYONYO?
Naacha!
Tulia na ZOUK LOOK- Pleure
Au tupate tu Wreck n EffeCT washauri utingishe TAKO katika RUMP SHAKER
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment