Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UMEMSAIDIA marehemu KUFA LEO?

>> Sunday, December 21, 2008

Labda....
.... ni kweli marehemu hahitaji msaada wakuendelea KUFA.

Na..
... kuna mengi tunafanya bila kufikiria mchango wake kwa YAI ni YAI kuwa YAI VIZA.

Yapo tufanyayo katika kujaribu kubomoa GESTI YA MAKUTI bila kustukia tunachangia sehemu sehemu pajengwe GUEST HOUSE ya ghorofa.

Na ni kweli...
... mfurahia paja la kuku ni amlaye MAREHEMU KUKU.

Na bado ni kweli...
...binadamu aliyemjengea banda BATA wa kufugwa, anaweza kusahau KUKU alikuwa anaishi bila KIBANDA , bila viatu, KABLA YA KUFUGWA.

NA NI UKWELI...
....mchango wa binadamu kwa kuku mwenye KIKOHOZI labda ni ugonjwa wa MDONDO.

Swali:

  • Pamoja na kutonielewa, UMEMSAIDIA MTU KUISHI LEO?

NAACHA!
_________________________________________________
Leo ni JUMAPILI hebu tukumbushwe NABII ISSA a.k.a YESU ingawa sinauhakika na staili ya wimbo....


Au GYPTIAN azungumzie MWANAMKE MZURI...katika BEAUTIFUL LADY

Au LUCKY DUBE azungumze MAPENZI katika.....I Want To Know What Love Is

AU tu GYPTIAN aendeleze mapenzi katika..I CAN FEEL UR PAIN...


JUMAPILI NJEMA!

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:51 am  

Jumapili njema nawe pia Simon-:)

Mzee wa Changamoto 5:12 pm  

Well!! Nikimnukuu Bushman katika albamu yake ya Higher Ground kuna wimbo aliosema "in order for one to survive, sometimes you gotta take another one's life". Na hata sisi twasema Kufa kufaana? Ama umesahau huo msemo? Ni ukweli usiopingika kuwa ndivyo dunia ijiendeshavyo. Yaani kama wanasema sisi twatokana na mbegu ambazo hutokana na vyakula tulavyo, unadhani yawezekana kabla hujawa wewe ulikuwa karanga ama korosho ambayo wazazi waliila kisha zikawa mbegu ukawa wewe? Kama kuna ukweli basi ni lazima ujue kuwa ilikuwa ni lazima Korosho ife na iliwe ili uje utuelimishe na kama hiyo mimea inategemea mbolea ambazo ni uozo wetu, basi yawezekana tukifa tukarejea kwenye mchicha (utakaofyonza samadi ya uozo wetu). Nami naacha maana sitaki kuamini kuwa nilishakuwa kitu kingine kabla ya hapa na wala sitaki kuamini kuwa nitakuwa kingine baada ya hapa. Yawezekana tulishawahi kuwa binadamu kabla ya sasa na pengine hii hali tuliyonayo sio ya ubinadamu wa mwisho. Labda tutarejea ena tukiwa binadamu baada ya kuwa mbolea ikanyonywa na mimea ikaliwa na watu tukawa mbegu kisha tukawa viumbe tena.

Ooooops!! Leo Jumapili natakiwa ni-stick kwenye imani na sio sayansi. Naacha

Unknown 5:28 am  

Ahsante kwa mchanganuo mzuri Mzee wa changamoto.

Ambiere, nimepita kibarazani kwako kuchota mawili matatu ili kuongeza ujinga wa kitu kinachoitwa elimu.
Bwaya aliwahi kusema kwamba kwa jinsi mwanaadamu anavyozidi kusoma ndivyo anavyozidi kuwa mjinga.
basi naomba nikiri kuwa nami pia ni mjinga, kwa sababu nilikubali kukaririshwa nadharia za watu waliokufa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 5:10 pm  

he ni kweli tunakula maiti za wanyama lakini mimi simo najitoa kabisaa kwa wanaokula maiti.

binadamu kwa kujitia wema eti tunafuga kuku bata na kuwapa maisha mema kumbe wangeweza kuishi na waliwahi kuishi kabla yetu

MARKUS MPANGALA 6:42 pm  

aaaaaah ha ha ha ha Kamala unajitoa nini wakati juzi nilikukuta ukifakamia ile kitu pale kijiweni kwako. au niseme samahani kumbe huyu yuko mjini. huku nyasa tunakula tena hasa wale waliokufa tena akija bwana mifugo anathibitisha salama TWALA kwani kuna kuna hiyana? mmmm sijaelewa soma ngoja nikomee hapa kwa leo. nimerudi tena wakuu malaria ni noma

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP