Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SWALA la WAAMINIO umasikini wa RAIS NYERERE kwa KUFARIKI bila BENZI la KIFISADI!

>> Wednesday, December 24, 2008

Umaskini wa mwenye ghorofa ATOSHEKAYE na KIBANDA, ni wa afaye na GHOROFA.

Na...
...tajiri wa KIMASAI mwenye katambuga, labda KATAMBUGA ni MOKASINI.

Udhanialo linakupa umaarufu kwa wadhaniao WEWE BABU KUBWA kwa kuwa UNABONGA UNG'ENG'E, linaweza kukukosesha MWANADADA wa KIPARE kijijini kwa ukosefu wako wa KITHEMBE kwenye lugha.

Swali:

  • Utajiri wako unausikilizia kwenye gari gani wakati utajiri ni baiskeli au baiskeli bomba mbili ya hamilton kama ya swala hauna?



Ndio....
.....wajuzi wa lugha hawawezi kukubishia kuwa neno fisadi linaweza kuwakilisha kitumbua kama kitumbua kingeitwa jina FISADI.

Na...
.... neno fisadi si msaada kama litalengwa kwa waliodakwa tu wakiFISADI na wadhaniwao mafisadi wakati fisadi analipa mishahara ya wachunguzao MAFISADI .

Tatizo ni...
.....wadhaniwao ni mafisadi ni wengi na labda si kweli ni mafisadi ingawa jamii yenye uchungu iko bize kutafuta wakumlaumu a.k.a ze FISADI, kutokana na hali halisi ngumu ingawa kwa mazingaombwe fulani kunaambao wananawili na labda KIFISADI.

Hapa sisemi kuwa akina Kikwete, Mkapa au Mwalimu wao Nyerere ni mafisadi , kwa kuwa sina uhakika na haisaidii kitu ikiwa mara zote ni kibaka ATAUAWA na sio FISADI.

Na....

Mungu amlaze mahali pema peponi Rais Nyerere, na kama hataki kulala anataka kwenda disko ,na iwe hivyo kwa angalau kutupa cha kufananisha wakati hali halisi kibano inatusababisha tumtafute MCHAWI FISADI.

Swali:

  • Hivi kipindi cha Nyerere hakukuwa na kibano ingawa waliozaliwa juzi walienda shule?
  • Wakati mafisadi wanatufisadi , kibano gani kizuri kuvumilia na RTC hakuna?
  • Katika wafisadi mia uwalalamikiao , ni mafisadi wangapi unauhakika na kuthibitisha WAMEFISADI?

    NAACHA!

    Ngojea tumpate Louis Armstrong aJAZIFAI katika Wonderful WORLD yenye UFISADI...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP