Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sasa NINIIiiiiiI? SI Kila mtu anapenda SIFA ingawa akupendaye anaweza kukusifia hata MWENDO wako kama BATA?

>> Tuesday, December 09, 2008

Ukisifiwa na adui , UMESIFIWA.
Ndugu, marafiki , na wakupendao, wanaweza wakakusifia sana hata kwa CHOGO LAKO kwa sababu wanajua udhaifu wako wakudhani una chogo kama NYUNDO.

Unaweza kusifiwa hata visivyosifiwa na wapendao ujisikie vizuri kwa sababu si siri, UNAPENDA SIFA hata kama unajulikana kwa SIFA ya kwamba HUPENDI MAKUU wala sifa.

Lakini...
..... sifa ni sifa, iwe ya uchapa kazi au uvivu.

Kumbuka....
.....Staili yako mpya ya kuloga, inasifa mbaya kwa WALOGWAWO, lakini inakupa umaarufu kwa wachawi WALOGAO.
Swali:

  • Unafikiri SHETANI atakusifia sana kwa UASHERATI au KUUA ikiwa vyote ni dhambi?

NAACHA!

SIKU NJEMA!
Kama unamuda msikilize tu Barry Schwartz: azungumzie MAZUGAZUGA YA binadamu KUCHAGUA kwa sababu kuna vya KUCHAGUA katika: The paradox of choice


AU tu MAXWELL anong'oneze katika NINABAHATI au Fortunate

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP