Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA umebanwa na VINUKAVYO, mahali popote ni CHOONI.

>> Thursday, December 11, 2008

Kila mtu ni STADI wa kutafuta pakujisaidia KICHAKANI, na katika ubunifu , majani, mchanga,jiwe au chupi , VYOTE ni VICHAMBIO.

Tofauti ipo lakini....
.......kwani , katika jitihada za kujaribu kusahaulisha UMATI kuwa umetoka KUJISAIDIA kichakani, KUNA WAPIGAO MLUZI.


Lakini....
...kama kuna aringaye , mtunza heshima wakati kukosa adabu hakudhuru, au adharauye, HAJABANWA HUYO!

Ukibanwa vyakula vyote VITAMU.
Ni UTU tu uzuiao MBWA kula MTU ndani ya KIBANO cha watu.

Swali:

  • Unafikiri wote wajiuzao wanasikia starehe ya kuuza chini ya KITOVU ili wapate vyakula JUU ya KITOVU?
  • Kwani nani hapendi raha akiona wasikiao raha hata kama raha yenyewe ni maumivu ya KUFUNGA?
NAACHA!
Topiki Imenishinda!
SIKU NJEMA!

Basi ngojea mtoto AMTAHADHARI mama yake ;''KWEPA WANAUME WEUSI'' katika Son Warns White Mom: Avoid Black Men

Au tutulie MSAUZI, Abdullah Ibrahim a.k.a DOLLAR BRAND aJAZZIFAI katika - Mannenberg

Basi bwana naacha ingawa YingYang Twins wanataka kunon'gona MATUSI[ usisikilize lakini kama utakwazika au kuingia dhambi:-(]

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 12:02 pm  

Najua chakula chenye afya hutoka udongoni (kwenye uchafu) na chenye afya njema tena kiitwacho Organic huwekewa mboji (kinyesi cha wanya ama uozo wa mimea). Ni kweli kuwa ili kufaidi vizuri ni lazima "uchafu" utumike? Labda tuangalie asili ya wanao ilivyo na kama unajivunia uzuri wake utembeapo naye, jiulize asili yake.
Nami Topiki imenishinda Simon

Simon Kitururu 1:13 pm  

@Mubelwa Mzee wa Changamoto:Ujumbe umefika. Tungekuwa tunachunguza asili , hakuna wa kumdharau mwingine.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP