Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA kukwepa KUKUMBUKA Simon Kitururu ataKUFA!

>> Wednesday, December 17, 2008

Kama bado sijafa , IPO SIKU na sekunde nitaKATA roho kabla au baada YAKO.

Mtu akifa tunastuka kama vile tulikuwa tunajua ni sekunde gani ataanza kivyake kwenda kunako bila viatu au kwa lugha maarufu KUFA.

Na...
....kujichulia si tabia nzuri hasa katika MILA na DESTURI za jamii kibao, ingawa mara nyingine kuna tusionauhakika na kujichulia ikiwa kuna aaminiye si kweli mtu akifikiria tu jambo la kisenge anaweza akajikuta kawa msenge.


Swali:

  • Lakini si kuna watu walikuwa wanajua muda wa Saddam Husein kufa?

Kuna mambo usijiombee kama unasababisha kuongezea maji juisi TAMU halafu ukifa kweli kuna watu wanaweza kufikiri stori za kufa kwako NI UTANI wakati ni kweli imekufa hata ukitumia VIAGRA.

Lakini...
... labda Simon Kitururu alianza kufa tokea kabla hajaona dunia, pale chembechembe hai mwilini ziumbazo binadamu ZILIPOANZA kufa ILI zipishe mpya baada ya LIJAMAA kumpa mimba JAMAA na ndio maana LIJAMAA chembechembe zinakufa na LINA mba.

Sibishi!
Kuwa hai ni bahati tu!
Swali:
  • Unajua ni bahati tu sisimizi hawakuingia masikioni na puani ulipolala jana na usingeweza kuzuia kwa sababu ulikuwa umelala?
  • Hivi ukifa utakumbukwa kweli , ikiwa wewe mwenyewe hukumbuki asilimia 98% za ndugu zako wa damu waliokufa hapa duniani ?


Samahani kwa kuwaza ujinga!

Lakini labda....
....nipo hai ndio maana naongea ujinga.

Si ujinga kufa ingawa inasemekana kunawaaminio kuwa kuna wafao KIJINGA.

Pamoja na kwamba niongeacho ni cha kijinga, NAKUTAKIA KILA LA KHERI katika kujisahaulisha TUTAKUFA!

Jiandae kama unajua jinsi ya KUJIANDA au UTAJISIKIA VIZURI kuwa angalau unajitahidi kujiandaa kwa kusali chini ya MBUYU!


NAACHA!

SIKU NJEMA kama UKO HAI!

Tupumzike kwa kuangalia KIFO......katika just for laughs-DEATH


AU PHIL COLLINS astue katika IN THE AIR TONIGHT


Nipo sijafa bado lakini ,kama unionavyo katika picha mbili tatu za juzi ya jana....
Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

AU tu William Baldé atuchangamshe kwa kibao Un rayon de Soleil

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP