Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

FURAHIA KRISMASI haraka haraka KAMA UNADHAMBI, Yesu asijerudi ghafla BURE kabla hujamalizia DHAMBI!

>> Wednesday, December 24, 2008

YESU akirudi SIKU YA KRISMASI kama wewe ni miongoni mwa waaminiyo ya Nabii Issa a.k.a Mwokozi, kuna watakaostukia zawadi za krismasi walizopewa na KUTAKA ,ni MATUSI.


Labda..
....krismasi ni nzuri kama inakukumbusha ya YESU na ufanyacho ilikufurahia kuzaliwa kwa YESU si dhambi.

Na..
... kama huamini ya YESU kwa kuwa ulistukia dini nyingine za wajanja wakutishao pia, kazi kwako kwa sababu inasemekana kwa waaminio; YESU ni MTOTO wa MUNGU mwenye huruma na NI MUNGU mwenye huruma asiyesita kukuchoma kama UNA DHAMBI.

ANZA KUFURAHIA!
Yesu anaweza kurudi kabla UBWABWA haujaisha!

:-(


Kama wewe unamchezo wa kuamini, TUBU ,SHAURI ZAKO!

Swali:

  • Hivi ubwabwa hautoshi katika kufurahia PASAKA mpaka utake nanihii?
  • Kwa waaminio , unachekelea zaidi kufa au kuzaliwa kwa MWOKOZI ,ndio maana una suti ya PENTEKOSTE?



NAACHA!
Niombeeni kama huwa mnakumbuka KUSHUKURU na sio KUOMBA TU , nisifanye dhambi siku ya Krismasi na ubwabwa upatikane!


Kumbukeni wasionahata chakusherehekea kutokana na maumivu ya kila siku ya kuchacha, magonjwa na hata wale wasahauo ukweli wa siku hii kuwa NI ya kubunia na labda yesu alizaliwa Julai kama Father Krismasi!

KRISTMASI NJEMA KWENU WOTE!

Tulia na STRAIGHT no CHASER waongelee KRISMASI.....katika....The 12 Days Of Christmas



Au tu tuendelee na ZOUK kutoka kwa JOCELYNE BEROARD aendeleze za - VINI SéRé

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 12:19 pm  

AMBIERE SALAAMU HIZI ZIMETULIA,
HA HA HA HAAAAAAA.........

Mzee wa Changamoto 4:23 pm  

Chichemi leo

Christian Bwaya 7:53 pm  

"..kama huamini ya YESU kwa kuwa ulistukia dini nyingine za wajanja wakutishao pia, kazi kwako kwa sababu inasemekana kwa waaminio; YESU ni MTOTO wa MUNGU mwenye huruma na NI MUNGU mwenye huruma asiyesita kukuchoma kama UNA DHAMBI..."

Hivi ni kwa kiasi gani dini zetu zinatueleza ukweli kuhusu Mungu? Niliwahi kusoma makala moja ya Ndesanjo Macha: Dini yako inakuzuia usimjue Mungu! Mungu anaelezeka kwa maelezo haya ya dini ambazo mimi hudhani nyingine hazijui hata anafananaje?

Anonymous 11:01 pm  

X-Mas njema kwa wote mungu ajaalie mwaka mpya ufike kwa salama amin

Simon Kitururu 7:41 pm  

@Ambiere Kaluse + Mzee Mubelwa Bandio: :-)


@Bwaya:Huwa najiuliza sana swala hili mkuu.Binadamu mwenye akili ananizingua kweli akizungumzia maswala ya imani yake kama ilivyopaliliwa na dini yake.

@Al-Rawahy Hilal a.k.a Mzee wa Taratibu: X-mas njema kwako pia mkuu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP