Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SIUJANJA kubishana na ALIYEJIANDAA na JIBU!

>> Wednesday, December 10, 2008

Aliyejiandaa na jibu , yuko tayari KUKUBISHIA.

Aliyejiandaa na JIBU, LABDA anajua unataka KUULIZA nini.

Aliyejiandaa na jibu anaweza kukuandaa uulize SWALI wakati unajua jibu.

Lakini...
....aliyejiandaa na JIBU utajua tu jibu lake ukimpa muda bila kumuuliza swali kwa jinsi MAJIBU yanavyo MTEKENYA mukichwa akisubiri ajibu.

Swali:

  • Umeshastukia atakaye kukunyima anavyokusubiria KWA HAMU umalize kuomba?
Lakini....
.....mbishi atakubishia hata ukweli ingawa kastukia JIBU LAKE halifanani na SWALI LAKO.

Na...
.....dunia haigandi na jibu la jana laweza likawa LILIKUWA sahihi jana na leo linahitaji MBOLEA ya chumvichumvi.

Tatizo ni...
..... mbishi hazuii ukuaji wa mimba kama MIMBA imeingia DODOMA.


DUH!

NAACHA!
SIKU NJEMA!

Tulia na rebecca malope alete za MUNGU katika - uyingcwele


AU tu Nusrat Fateh Ali Khan aendelee kumsifu ALLAH katika - Allah Hoo

AU turudi tu katika ZA zisizojali mitazamo ya DINI a.k.a za PENDO LAKIBINADAMU kupitia kwa Onyeka Onwenu na MFALME wa JUJU MUSIC a.k.a King Sunny Ade waongelee maswala ya KUSUBIRI KANYAU katika: Wait for me.....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 6:03 am  

Mimi naona ni bora kukaa kimya kuliko kumuuliza aliyejiandaa na jibu.

kwani kukaa kimya pia ni jibu kwa aliyejiandaa na jibu kuwa huko tayari kupokea majibu yaliyoandaliwa kabla ya swali linalohitaji majibu makini.

Ukweli ni kwamba sihitaji majibu kama yale ya bungeni anayoandaliwa miezi kadhaa kabla ya kikao.

Sihitaji majibu.

Simon Kitururu 8:05 am  

@Mzee Kaluthe:Nakubali kabisa Mkuu!Asante kwa kunitembelea Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP