Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA staili ya NGONO , mwerevu imempa GONO!:-(

>> Thursday, December 04, 2008

Katika maono,
....nitakacho ni dhambi ingawa KINONO.

Sitangazi mgomo,
...wajua siri,kama wewe navizia nono.

Tungefunzwa mauno,
.... labda peni kwenye TUNDU ingemwaga wino.

Karatasi lenyewe NONIHINO,
...kufuta ni KUJIPAKAZA na kupakaza WINO.

Najifunza MUMO kwa MUMO,
.....werevu wan'teta udhaifu MGUNO.

Mwerevu an'nyima somo,
....
hapendi kwenye bata firigisi ilimo.

Mwerevu mjuaji mno,
-Ni uerevu kumnyima mwenye kundu KUNYA MNO?

Kama mjua PANYA mkata KIUNO,
-si ni uerevu kun'funza staili za kula panya MNONO?

Kama kidaka tonge kina meno,
....n'stue za kuchovya bila kung'atwa meno.

Kama staili zina udenda moto mno,
.......n'stue nivae glovu na sio chupi au kimono.


LAKINI....

Mwerevu ana SIRI na kisonono,
... hajulikani kwa KIDONDA NDUGU, MDUDU ,wala GONO.

Kukana mahiri mjanja mno,
..binadamu humsifu ,kwenye kosa yeye hayumo.

Atukataza tusifanye nono,
... akijua lazima tutaonja humo!

Badala ya kutufunza somo,
....adai tuvumilie na ni sumu unono.

YEYE afanya MPAKA konokono,
....atunyima somo na hafuati ajualo somo.

Mtaalamu MWEREVU, mwenye NGOMA na somo,
- mbona BADO wafa na GONO?

:-(
------------------------------------------------------------------------------------------------
NAWAZA tu MKUU!
Siku NJEMA !

Tupewe funzo kidogo na TENDER MVUNDLA...

Au twende tu NIGERIA kumsikiliza MAJEK FASHEK.......katika So Long TOO LONG

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP