Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA kunahitajika MAPINDUZI ya mnyonge KUACHA kumpigia makofi MHESHIMIWA pipi.

>> Thursday, December 18, 2008

Labda...
.....ni kweli BIN-ADAMU wengi hupenda kuongozwa ndio maana kuna KIONGOZI wa VIONGOZI hata katika ujinga.

Unaweza KUBISHA!

Lakini...
....wanyonge ni kiboko kwa kushangilia WAHESHIMIWA hata kama ni wezi wa nyeti kinuka mkojo kama tu Kawawa na Mkapa kama sio Kikwete na Mwinyi wamsifiavyo Nyerere kwa azimio la ARUSHA lililokufa WASILOLIFUATA.

Hukawii kusikia sifa KEMUKEMU za KIONGOZI wetu zimzidivyo kiongozi WENU hata kama KIONGOZI WETU anamsaada ZAIDI kwao kuliko msaada wa kutuibia KWETU .

Ganzi KIYOYOZI ipatikanayo kwa kumpigia makofi mtu hata kwa usichokielewa kwa sababu ni MHESHIMIWA kada wa chama chako , kinamna , ni kama kuwa na mapoozeo ndugu, MKIZAA mtoto ni KILEMA.


Inasemekana kuna visababu LUKUKI kama vya tamaduni, elimu, dini, NJAA au na kadhalika tano na nusu , viongezeavyo UMAARUFU wamwenyenacho KIONGOZI wetu, KWETU.

Lakini.....
...wenye nguvu ni wanyonge walio wengi kama wakiamua KUDINDA kiongozi asidinde.

Lakini....
..... shangilia tu ili uongozwe !

Swali:

  • Si ndio maana kuna GWARIDE umshangilie MREMA kama Mtikila ingawa Kikwete ndio chekibobu?
Naacha, topiki imenishinda. :-(

Tulia na BECK wanisaidie katika spirit ya KUSHINDWA katika kibao LOSER.....


Au tu mwanadada akumbushe maswala ya KIJINGA au MAANA kama KUOSHA katika WASH ya ASS...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP