Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Swala la UJANJA ni kusikiliza MIZIKI topu teni!

>> Friday, December 26, 2008

Kuna wadaio miziki mizuri iko topu teni!

Na..
...wakipenda labda penda kwa sababu WANAPENDA ingawa wapendacho kama ni BEBERU ,basi anapenda KUNUSA mpaka uvundo wa sehemu za haja kubwa za mbuzi inagawa sehemu hizo kwa mchoma nyama labda sio shilingi teni.


Inasemekana umaarufu wa kitu topu teni ni kwa sababu masikioni mwa wengi ni bomba.
Ingawa swala hili laweza kukufanya ujiulizea pia mchango wa video zisindikizao muziki hufanyanini katika kuufanya wimbo mzuri wa mazishi uwe bomba harusini.

Na nikweli..
....miziki mizuri ya dini utaisikia mpaka kwenye vilabu vya pombe Uchagani kama tu ile ikatazayo uzizi ipigwavyo kwenye gesti ya jirani.

Swali:

  • Kwani miziki mizuri ni ile tu uisikiayo redioni?
  • Hivi unafikiria ni kwanini kuna wapendao hard rock na wapendao ngwasuma?
  • Unauhakika hujashawishiwa kupenda miziki uipendayo na labda mlio wa mbuzi kwako ungekuwa mziki tosha?



Lakini.....
.. miziki topu teni ya Baba , labda kwa Babu ilikuwa makelele masikioni.

Na ...
... miziki mingi rahisi ndio hua maarufu kwa wengi ndio maana iko topu teni.

Na labda ...
... kama wewe ni mpenda miziki iliyo topu teni, inawezekana unapenda vitu rahisirahisi kama maharage ya Mbeya, na usishangae KISAIKOLOJIA kuwa, wewe si mvumilivu na labda mvivu hata kama ni mvivu wa kusukuma mkokoteni.

Lakini...
.. Chekibobu na SistaDU labda waonekana wajanja na ni maarufu KWENYE PATI kwa kujua miziki topu teni!

Ila..
.. ukifikiria sana , inawezekana miziki upendayo umechaguliwa na sio chaguo lako kwa sababu wewe mvivu na usikilizacho ni usikilizwacho na ndio maana kwenye pati yetu ya kunema usipokuja labda tutapata ahueni.

Swali:

  • Ushawahi kusikia mziki kwa kumsikiliza aliaye?


Samahani naenda kukojoa!
Baadaye!


Au pata kidogo muziki wa Eartha Kitt ambaye ametutoka jana . Pamoja na kwamba alifanya show Afrika Kusini kipindi cha ubaguzi wa rangi , R.I.P Eartha...

Asante kwa wimbo huu Santa Baby

Au tu turudi Kenya kukutana na Safari Sound Band watuletee ya MPENZI ,kwa sauti ya kubaniwa pua....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 12:17 pm  

Hahahaha. Ni kweli. Si waona namna tunavyothamini vitu vionekanavyo kutoka "matawi ya juu" hata kama si chaguo letu? Tunakuwa kama mihogo iliyopikwa ikagoma kuiva na unajua kuwa hiyo hailiki. Yaani muhogo m'bichi (wacha niufananishe na maisha yetu) walika na ni mtamu sana, na muhogo uliopikwa ukaiva (niufananishe na maisha ya wenzetu) unalika na ni mtamu pia. Lakini kwa kuwa tunataka kuwa kama wenzetu na mazingira hayaturuhusu na hayataturuhusu kuwa hivyo, tunaishia kuwa kati kwa kuupoteza u-sisi na kutofikia u-wao matokeo yake tunakuwa kama muhogo uliopikwa na usiive (na huu hauliki). Shauri yetu na hizi NDIO MZEE hata kama hujasikia swali uliloulizwa. Kupenda tusivyopenda kwa kuwa tumdhaniaye ana busara anavipenda. Kumbe twadhani ana busara kwa kuwa hatujibusarishi wenyewe. Si wajua hata ndani ya wajinga kuna mwerevu? Haya sasa kwa uvivu wa kufikiri na uzembe wa kujitambua twamfanya mtu afikirie kwa niaba yetu kisha tumhsangilie na kumshabikia. Nilikutana na mwana Bongoflava kavaa jacket ya leather nyumbani na joto kali lile (nadhani alikuwa anavunda kwa ndani) kwa kuwa tu "fulani" mwenye chati huko majuu ame-shoot na jaketi la hivyo. Ndio top ten zenyewe. Naacha (japo si kwa sababu kama zako) niwape nafasi waonao tatizo hili kwa "angle" nyingine

Simon Kitururu 1:15 pm  

@Mzee wa Changamoto: Kazi ipo! Vipi X-mas inaendeleaje?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP