Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WASTAARABU katika kujifanya hawamuelewi MWANADAMU atoleaye macho WALIOVAA uchi!

>> Wednesday, December 17, 2008

Wastaarabu wanaeleweka!
Swali:

  • Si wana tabia nzuri?
Tatizo ni...
...pale tabia nzuri zijengapo UNAFIKI.

Unaweza ukajikuta unakufa KISABUNI kwa kuishi kwa kujitutumua hupendi ukoko wakati mzimu wako ni wa UTANDU na UKOKO katika starehe ya WALI.

Mila , desturi , dini au mpaka tu staili yako binafsi ya kukwepa harufu ya mavi hasa KAMA WEWE ni MHESHIMIWA, inaweza kukujengea au kujengea mpaka jamii yako MIIKO ya ambavyo si MWIKO.

Swali:
  • Hivi ushawahi kumshangaa padre au PAPA JOHN PAUL kwa kuvaa gauni?
Lakini...
...Unaeleweka,Una TABIA nzuri!:-(

Tusiwe wanafiki lakini!

Binadamu kibaologia ameumbika atamani kuchungulia hasa kwa sababu pachunguliwapo pana AHADI za KUZALISHANA kitu ambacho binadamu ni shujaa hata uwaweke kwenye kambi ya WAKIMBIZI kwenye njaa, vita na hakuna KICHAKA GESTI.

Lakini ...
..... jamii imenifunza tabia nzuri na labda itabidi nikushangae kwa KUDOKOA wakati jamii nzima inajua UNANJAA na chakula haikupi:-(

Tatizo sugu ni...
.....labda JAMII nzima inaishi kinafiki ndio maana asiyemnafiki JAMII inamtambua kama KIBAKA au KAHARIBIKIWA na anatabia mbaya kwa kuchungulia ANYIMWACHO!:-(

Topiki IMENISHINDA!
NAACHA na natumaini unajua NAWAZA tu hapa MKUU!
SIKU NJEMA!

Ngojea TUPUMZIKE kwa kumsikiliza mwanadada ashauri WANADADA katika Black Women Should Date Outside The Race

Au David Blane atoe TU moyo wake katika Heart Exposure(Usiangalie kama unaogopa damu au mtoto)


Au tu TONI BRAXTON aseme LET IT FLOW

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 10:13 am  

kibaka kaushinda unafiki au sio? hii sasa kali, ndo maana mafisadi ni washindi na vibaka ni wabaya, sio wanafiki

Simon Kitururu 10:30 am  

@Kamala:Vibaka naamini kwa asilimia kubwa wanalazimika kuwa vibaka ukifananisha na ulazima wa fisadi kuwa fisadi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP