Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jifunze SIASA YA UJAMAA, ikusaidie kufaidi UBEPARI!

>> Friday, December 19, 2008

Utamu wa chachu husaidia kujua kwanini unaridhika na UTAMU wa BWIMBWI kama tu ukinaivyo uiitayo TAMU na si chachu.

Na...
...ukiwa nje ya kiwanja , unaweza baadaye kupata mdadi wa kuingia ndani ya kiwanja kwa nguvu zote na mara zote kwa kudhani kunakitu ulikuwa unakosa ULIVYOKUWA nje ya kiwanja ambako shoo yenyewe haikuwa ya YESU.

Swali:

  • Si Michael Jackson kwa kutochezea madoli utotoni , bado ananunua madoli ya kuchezea ukubwani?

Ujamaa MTAMU kwa sababu kuna iwafanyao kudhani walikosa ubepari kwa kuwa ndani ya UJAMAA.

Kuna stori nzuri za UJAMAA za kukuhamasisha kuwa bepari kama ukisikia :
  • Kuna watu hawatasita KUkuBEPARI kwa sababu wanadhani wanajua kwanini SIASA YA UJAMAA jinsi ilivyo washinda WANA SIASA YA UJAMAA kama Rais Mkapa, Kikwete na wengineo kwa nguvu zaidi BAADA ya Nyerere kufa kama tu KAMBONA kabla ya Nyerere kufariki.
  • Waziri Mkuu Sokoine alijitahidi kabla ya kufa kutunza maadili ambayo baada ya yeye kufa YALIKUFA NAYE katika mtiririko uliohakikishia umati HATA azimio la Arusha lilishaanza kufa.

Na tunasikia:
  • Wengi hata hawamkumbuki mchapakazi aliye kuwa anahakikisha kisemwacho kinatokea aitwaye KAWAWA , ambaye alifanikiwa kusababisha utekelezaji wa uwepo wa VIJIJI vya UJAMAA mpaka baadaye kidogo wajanja walipostukia staili za CHAKO CHANGU , CHANGU CHANGU.
Lakini.....
....siasa ya ujamaa ni ugonjwa tu kama ubepari umetibu matakwa ya Kalumekenge.
Kwa asiyepona kwa ubepari ,UJAMAA bado ni dawa kwa Kalumekenge.


Labda...
.... tatizo liko pale tu watu wasahaupo kuwa dunia haigandi na mfumo wowote ukimaliza kuuandikia kitabu kama Nyerere, labda MFUMO ushaanza kupitwa na wakati na unahitaji umakini wa kukimbia nao kwa kustukia hali halisi ambayo inaweza isiwe ni mfumo wa ubepari wala wa Kijamaa andunje, ukila nao bega kwa bega.

Lakini...
.....Labda jifunze UJAMAA!
SI ubepari unakuja kirahisi kupitia hulka ya KIBINADAMU ya UCHOYO na UMIMI?


AU?


Samahani naenda kukojoa!
Baadaye!




Ngojea tu TONTO IRIE adai IT a RING


Au nimuachie Lokua Kanza na WENZAKE , Live in South Africa...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP