Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nashughulikia kaudhaifu KAKUSHINDWA KUACHA kutaka KUKUMBATIA!

>> Tuesday, December 02, 2008

Kama hujawahi kukumbatiwa labda ushawahi kufanikiwa kukumbatia MTO.

Kubwa zima unaweza kulistukia linasikia raha kwa sababu limekumbatiwa!
LOH!

Swali:

  • Kwanini unakumbatia?
Labda.....
....kama unafurahia kukumbatia ,basi unakaudhaifu kakutaka kuwa karibu na mtu umkumbatiae, iwe ni ndugu , jamaa, rafiki au limtu ambalo ungetamani hata kulikumbatia wakati limevua VAZI.

Inasemekana kukumbatia kunasaidia mvujo wa hormoni ya OXYTOCIN, isaidiayo katika kukuza ukaribu wako na LIMZAZI lako, Litoto, Lirafiki lako au Limtu lolote MPAKA katika maswala ya KUAMINIANA.

Lakini ...
... pamoja na kujijua unapenda kukumbatia, inawezekana kuna limtu unakwepa kulikumbatia.
:-(

Baadhi ya vitu ambavyo mara nyingine nahisi vinachekesha kama kuna kiumbe kisicho binadamu kinashuhudia WAFANYAYO binadamu baada ya kupumzika KUPIGANA vita au angalau kumteta asiyepo kwenye kikao; ni kuwachungulia binadamu wakati wasikishwa raha kwa kitu kidogo KAMA kukumbatiana.

Kuna jamaa utalistukia linasikia raha hilo likikumbatiwa mpaka linasahau kwa MUDA kidogo kuwa linadaiwa kodi!

DUH!
MIMI siyo mtaalamu sana wa kukumbatia , ingawa na jaribu kuendeleza kufanyia mazoezi kukumbatia,kila nikipewa nafasi hata na MTO, labda ndio maana topiki hii imenishinda.

Lakini...
.... nahisi kama unafurahia MKUMBATIO basi una UPWEKE hata kama ni wa kitu usichokistukia sasa hivi mpaka baadaye.


BAADAYE BASI!

Kumbatia sasa hivi kama inawezekana!

Baadaye unaweza ukawa huna MIKONO!

'PUUuH'; Nimetema mate chini na kugonga mbao kuepusha NUKSI ;nisije nikakosa KUKUMBATIA bure!:-)

SIKU njema na msalimie ujisikiaye KUMKUMBATIA!

Twende NIGERIA kukutana na P SQUARE walete za DO ME


Au tu Rihanna na Sean Paul walete za -BREAK IT OFF wakati tunaendeleza LIBENEKE...

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:39 pm  

Simon, Ni hivi mimi ninavyoelewa ni kwamba kukumbatiana ni aina ya kugawa furaha na uchungu. Wote tunahitaji kukumbatiana kwa sababu tunajaliana. Kuanzia bibi mpaka yule umpendaye, kukumbatiana ni kitu cha kustajaabisha (kizuri). Ni njia ya kuonyesha upendo bila maneno. Ni ajabu kuona kukumbatiana kunawapa watu furaha. Kukumbatiana kunafaa kila mahali kwa lugha zote. Kukumbatiana hakuhitaji betri, kwa hiyo sasa inachobidi ni kuendeza mkumbato na mpe rafiki yako/zako na yule umpendaye. Haya mimi naanza tayari sasa hivi nimesha kukumbatia:-)

Simon Kitururu 1:16 am  

@Yasinta:Sina uhakika kuwa tamaduni zote zinaruhusu kukumbatia. Unaweza kumkumbatia au kumbusu mtu ilikumsaliti kama alivyofanyiwa YESU kwa waaminio simulizi za biblia.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP