Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASIYELEWA katika UJUZI wa kwanini MLEVI kalewa!

>> Monday, December 15, 2008

Ingawa profesa ujuzi hewa,
......aheshimiwa na cheo kapewa.

Kashaendelea MHESHIMIWA hajalewa,
.....ndio maana haelewi waliolewa.

Ujuzi wa moja si lazima mbili waelewa,
.....ingawa sifa ni pombe waweza kulewa.

Cheo kipo ndio maana profesa hewa,
.....hisabati na dini MTAALAMU anaelewa.

Kabatizwa kwa moto na sio hewa,
...msikitini afunzwa JINIPEPO si hewa.

Katika jamii aileayo alilelewa,
...na nyumbani watoto alelea.

Walelewao SIRI ya profesa wamsifiaye wangeielewa,
....Mjinga asingechekwa KALEWA.

__________ ______________________ _______________________
NAACHA!
Swali:

  • Hivi mara zote sababu ya mlevi kulewa, si ni kwa sababu kanywa pombe ili alewe?

Nawaza tu MKUU!
Jumatatu njema!
Au ngojea tusikilize mjadala TV yaKUSAIDIWA KUJIUA katika British debate: Suicide on TV?


AU TITI kutoka SENEGAL atuburudishe kwa kibao ...- J't'aime

Nimuachie TITI tena atafsiri wimbo wa BOB MARLEY katika staili ya MBALAX...katika kibao kiitwacho Tayumako....

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:10 am  

Simon! Kazi kwelikweli, Ama kweli unawaza mbali sana!Nasema kama Edo asemavyo tutafika tu!

Unknown 5:25 am  

AMBIERE NIMEPITA KIBARAZANI KWAKO LEO ASUBUHI SAA 12 NA DAKIKA 30 ASUBUHI!!!!!
KAZI NZURI MZEE, KAZI IMETULIA.

Simon Kitururu 7:53 am  

@Yasinta:Tutafika tu!Asante kwa kunitembelea na kunipa moyo Dada.
@Ambiere:Asante kwa kunitembelea mpaka katika mida ambayo kishumba kimepoa:-)Asante sana Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP