Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MKAO wakusubiria BIKIRA iondolewe!

>> Friday, December 05, 2008

Kuna watulivu!

Na...
...labda bikira inakera ingawa kuna bikira WATAKATIFU!

Labda....
..kila mtu anajua MTU alizaliwa BIKIRA, na labda bado ni bikira ambaye awezakufa na kutoenda PARADISO kwa kutoondoa angalau bikira ya DHAMBI YA ASILI, kama anafuata dini ambayo inakustua kamchezo ka KUZALIWA na bikira ya DHAMBI YA ASILI.

Tatizo la kuwa bikira ni kwamba, pamoja na KWAMBA unafurahia UBIKIRA WAKO wakuwa hujaonja wala kuonjwa, umaarufu wa UBIKIRA HUJULIKANA na labda kukupa nafasi yakuonyesha maringo yako DINGILIDINGILI mpaka chini, WATU WENGINE WAKIJUA kuwa wewe bikira.


Kwa jinsi abenjuavyo macho kwa kutazama muhogo , kwa tusiojua tunaweza kuamini Mwanaidi kama Prince Charles ni bikira wa muhogo wakati kwa kula CHIPSI DUME Chaupele kasingiziwa.

Swali:

  • Hivi wewe NI bikira wa kudokoa nanihii?

Kuna wavumilivu katika mkao wa kusubiria MAUMIVU kama ahadi ni UTAMU.

Binadamu akiaminishwa na DANGANYA TOTO kubwa kuwa KUNA UTAMU baada ya maumivu yakuchokonoa hata MENO, kama anapenda TAMUTAMU atajaribu kuonja CHUNGU ili kujaribu kufikia DANGANYA TOTO tamu hata kama ni TAMU KWA MUDA.

Kumbuka....
...watu WANATAHIRIWA hata kwa hiari kwa ahadi TAMU, hata kama ni AHADI zitimizwazo migombani , ili kupata kautamu katambulikako na JAMII hata kama ni jamii iaminiyo KUNYA si UTAMU.

Kumbuka....
... kuna waponao maumivu au WAPATAO NAFUU kwa sababu ya imani TU kuwa CHUMA MBOGA ni sahihi zaidi katika kuchuma UYOGA na NJEGERE ingawa kuna vichumwavyo pasipo MIMEA.

Swali:
  • Ushawahi kukaa mkao wa kufumbia macho uchungu kabla hujaonja UCHUNGU?



Wakati unasubiria bikira ya ujinga iondoke , inaweza ikawa ishaondoka ingawa bado unasubiria kwa sababu ni mpaka wengine waseme HUNA BIKIRA.
Swali:
  • Kwani ni lini tokea uzaliwe ulistukia kuna kitu kiitwacho BIKIRA?
Na...
..labda kuna wajitoao BIKIRA HII wenyewe bila kustukia bikira hii imetoka na ile BIKIRA YA SABA itakuwepo mpaka juzi ya MWAKA KESHO.

:-(

DUH!
NAACHA!
Topiki IMENISHINDA!

IJUmaa NJEMA na wikiENDI NJEma!

Lakini labda....
......Tufurahie tena Tanzania kwa kuangalia TANZANIA katika DARWIN'S NIGHTMARE TRAILER...


au tu Isaac Hayes aongelee CHOCOLATE SALTY BALLS
au ngojea turudi tu KONGO kwa MBILIA BEL alete za SENDA.......

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:47 am  

Lbada swali la kijinga itakuwaje Bikira maria aitwe Bikira wakati yeye ni mama wa mungu(yesu)?

ijumaa njema pia na pia wikiend njema

Mzee wa Changamoto 11:32 pm  

No comment. Asante kwa yote Simon

Anonymous 6:31 pm  

kazi kweli kweli...haya huyu ndio yule mdau wako wa tampere..utanikumbuka najua...

Simon Kitururu 10:51 pm  

@Yasinta:Swali lako gumu ingawa ni rahisi kama kuna MKRISTO.
@Muzee wa CHANGAMOTO: Asante Mkuu kwa yote na kwa KUTO nitenga.
@MUDAU: nakumbuka na ajsante kwa yote na ya juzi ya jana.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP