Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hakuna MATIBABU ya kuponya HAMU YA KUTUKANA kama tu kusivyokuwa na matibabu ya KUCHEUA.

>> Tuesday, December 16, 2008

Kuna wakutukanao bafuni na sio sebuleni!

Cha kushangaza...
....wengi wakasirikao baada ya KUONJESHWA tusi, hawafikirii undani wa tusi.

Kuna wengi wanakutukana kama akutukanaye UMFAHAMUYE.
Akutukanaye UMFAHAMUYE kuna kitu tu KABAHATIKA kama kukufikishia TUSI iliujisikie ambavyo watu kibao kadhaa WANAJARIBU kukuhamasisha UJISIKIE.

Utamu wa tusi ni pale atukanwaye anakasirika hata kwa matusi yasio na maana sana kama UNA KIIOO, kama:

  • Kichwa kama pua!
  • Mbwa wee!
  • Mdomo kama kinyeo cha bata!
  • ....na nakadhalika kadhaa mbili ZA MATUSI na nusu.
(SAMAHANI kwa MATUSI, na nitajitahidi kunawa mdomo !)

Sasaa....
....Naamini kuwa tunakasirika tukitukanwa kwa sababu tumeshushiwa heshima.
Lakini...
....mara nyingi heshima inaongezewa sifa na uzito hata usio wake, na mfano mzuri ni wale usiowaheshimu walivyo kuwa WAHESHIMIWA katika jamii ingawa kwa wizi ni namba moja ndio maana wengine ni WABUNGE au mawaziri wakisubiria URAIS kama tu WALE WENGINE wajulikanavyo kwa kuhubiri dini wasizofuata maadili yake.
Swali:
  • SI unakumbuka AKUTUPIAYE KIATU Iraki , ni sawasawa au ZAIDI ya akutukaniaye tusi la nguoni TANZANIA?

Nakubali...
...kuna matusi yanauma hasa yale yalengayo vikojoleo vya wazazi wasiohusika katika ugomvi wangu au wako na lijamaa wa nani mjinga zaidi.

Lakini ....
....kuna mahiri wa fani ya kutukana.

Kama tu katika fani kuna wenye hamu mpaka wanaweza kutongozea mistari ya KORAANI au BIBLIA ili wapate angalau KASHATA kama sio kupata UAMINIFU WAKO, wako wenye hamu ya kukutukana tu kwa sababu binafsi na wanajisikia ahueni kukutolea mvuke wewe Binti Maimuna kama vile tu Rais KIKWETE.

Hakuna matibabu ya hamu ya kutukana, na labda kama dini zenu zinaruhusu kutubu , TUBU tu kwa hamu ya kutaka kumtukana mzazi wako KWA KUFUNZA ADABU ,kama tu dereva wa daladala , kisa hakuelewi na hafuati sheria za TRAFIKI za mbuzi.

Labda hupendi MATUSI ingawa mara moja moja unajisikia kutukana!
Kumbuka ufanyacho ukitukana na watu kusikia umetukana ni kitendo tu.

Tusi ulisha tukana MOYONI na nia na sababu za kutukana zipo tu moyoni ingawa hujasema wala kufanya kitu.

Swali:
  • Umtukanaye anaelewa UJUMBE nyuma ya tusi?
  • Uliyetukanwa unakasirikia tusi au UJUMBE nyuma ya tusi?

Naacha TOPIKI imenishinda!
SIKU NJEMA!

AU tupumzike kwa kushuhudia Rais GEORGE BUSH akipewa tusi LA NGUONI kwa kurushiwa viatu......


AU DIDO ashukuru katika.. THANK U.

DUH!
Turudi tu AFRIKA kwa KING SUNNY ADE ambaye ndiye MWANAMUZIKI wa JUJU MUSIC nimzimiaye katika fani , kwa mara nyingine atupe AFRICA and AMERICA......

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:03 pm  

Simon! hapa ipo kazi na kweli hapa inatakiwa kuwaza hasa maana mmh kazi kawelikweli kama mimi nina maswali magumu.Basi wewe una mawazo magumu kazi nzuri Simon! karibu tena

Christian Bwaya 1:15 pm  

Nimepita kukusalimia kaka. Hatuonani siku hizi

MARKUS MPANGALA 6:02 pm  

kweli akutukaye hakuchagulii TUSI na akikuchagulia TUSI ujue hilo siyo Tusi bali anakusabahi tu. Na akutukunaye kama hajakusonya basi hajui mitindo ya matusi ni sawa na anayekutusi bila kuongeza maneno ya haraka haraka. ni sawa na yule anayetukana huku analia mwenyewe. PENGINE tusi kwa Joji Kichaka lilikolea baada ya jamaa kuona kakwepa viatu na wenyewe wanadai hilo ni tusi maridhawa tena litokalao na imani. Mweeeee pengine hatukujua kama Joji Kichaka anajua kukwepa matusi, na lakini akasema kiatu ni namba 10. Labda anajua kwamba TUSI lile ni cha mtoto huku wenye maaana zao wanajua katukanwa hata kikojoleo chake. heee imenishinda lakini BUSH atajifunza kutokwepa na kuanza kutukana kwa kutumia mdomo wake wa mjusi

Unknown 6:42 am  

AMBIERE HAKUNA KITU KINACHOITWA MATUSI, BALI SISI HUWA TUNATAFSIRI VIBAYA.

HIVI MATUSI NI NINI?

MATUSI NI LUGHA INAYOWAKILISHA VITU FULANI, KAMA VILE MAJINA YA VIUNGO VYA MWILI WANYAMA AU HATA MITI, AMBAYO SISI TUMEFUNDISHWA KUWA HAYO NDIO MATUSI.

HIVI BWANA KITURURU, NIKIKWAMBIA "LALALIKO" UTAKASIRIKA?

NAAMINI HUTAKASIRIKA KWA SABABU LALALIKO HAINA MAANA YOYOTE, NI NENO TU NIMETAMKA, LAKINI PIA INAWEZEKANA KABISA KUWA HUENDA MIONGONI MWA WASOMAJI WA BLOG YAKO WAPO AMBAO KWA LUGHA YA KABILA LAO NENO HILO LIKAWA NA MAANA YA KITU KINACHOITWA TUSI KULINGA NA LUGHA YAO.
SISI TUMEFUNDISHWA KUWA KUNA LUGHA YA MATUSI, NA TUMEONA WAZAZI WETU WANVYOFURA KWA HASIRA LUGHA HIYO WALIYO IITA MATUSI IKITAMKWA MBELE YAO.
ILI UJUE KUWA TUSI NI TAFSIRI, HEBU ANGALIA TUNAVYOBAGUA.
NENO HILO AKILITAMKWA NA MWENDAWAZIMU ATAPUUZWA LAKINI AKITAMKA MTU MWENYE AKILI ZAKE TIMAMU MTU ANAKASIRIKA.
HIVI NI KWA NINI?

AMBIERE NI HAYO TU

Simon Kitururu 10:27 am  

@Yasinta: Sijawahi kuwaza kuwa na mawazo magumu. Mimi mara nyingi hufikiria vitu vidogo sana kama kujikuna upele, kula, kukohoa nk!
@Bwaya: Mbona nipo kijiweni kwako kila siku?Sema sikunyingine nasoma kazi zako za miaka ya nyuma na nasikohoi kwenye mada mpya!
@Markus : :-)

@Ambiere: Kazi kwelikweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP