Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nyuma YA KICHEKO cha MWENYE shida ya KUNANIHII au NANIHII!

>> Wednesday, October 29, 2008

Labda shida ni tatizo!
Swali:

  • Nini kipimo cha shida ya mwenzako?

Wakati wa shida raha ipo tu ingawa imezidiwa na shida.
Wakati wa shida ingekuwa ni bomba la ujanja kwa mjanja kustukia raha iliyoko chini kidogo ya kipele isubiriayo umalize kuteseka na shida.


Labda Kisaikolojia , inawezekana kuna shida unaipendelea .


Labda....

Ukiona mwenye maumivu anacheka, kuna visekunde kaondoa fikirani katika kiini cha maumivu.

Kuna kipindi masikini hakumbuki umasikini wake kama tajiri awezavyo kutostukia utajiri wake wakati anakufa na kastukia haondoki ng'o na ligari lake mkweche au lile jumba la fedha za wizi.

Kuna kipindi unaweza kucheka baada ya kuanguka kitu ambacho ni kinyume na matarajio ya washuhudiao jinsi ulivyoanguka pale sokoni.

Kuna kipindi unaweza ukamcheka mtu kaanguka kabla ya kustukia kuwa amekufa baada ya muanguko.

BAHATI mbaya......

Kila mtu anashida na labda shida yako ni kubwa kuliko yake kama YEYE aonavyo shida yake ni kubwa kuliko yako.

POLE kwa shida yako!Mwenzio chamoto nakiona na shida yangu!

Baadaye basi!

Tulia na Morgan Heritage wakukumbushe Jamaica kama unaweza kufananisha na hali ya TANZANIA katika wimbo KUNA KITU CHAKUKUFANYA UTABASAMU au Nothing To Smile About


Au labda kuna waonacho cha kutabasamu kama Tony Matterhorn katika DUTTY WINE

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP