TUNASAHAU faida za SIRI ya ASIYE na MPENZI au TUSIYEMJUA kuvaa chupi SAFI!
>> Thursday, October 16, 2008
Jambo lako binafsi zuri si lazima likae uchi  kwa jamii kushuhudia , kwa jamii matunda yake kushuhudia.
Kitu ambacho hata hakijulikani, chaweza kuwa ni chanzo cha wewe kunichekea au hata kuwa na muda wa kunisaidia , kumsaidia ,kama sio kunionyesha chumba cha kujisaidia.
Tusichojua kikusumbuacho , chaweza kusababisha uwe mkali bila sababu katika  kiwanja cha penzi .
Unawezaficha siri kwa kujifanya mzuri, lakini mficha siri hufanikiwa kuficha siri kwa yule tu ambaye  si makini.
Siri yako  ya KUBANA KIJAMBO, yaweza kujitokeza kwa utofauti wa staili yako ya mkao kwa akujuaye.
Siri yako ya kubana mkojo , yaweza kujitokeza katika mwendo wako wakwenda msalani kwa akujuaye.
Siri yako wakati unaongea na mpenzi wa siri , inaweza ikawa katika staili yako ya kunong'ona kwenye simu huku ukijichekesha katika visivyochekesha.
Siri yako wakati unadanganya , inaweza ikawa jinsi tu unavyosisitizia hoja kwa akujuaye.
Sasaaaaa.......!
Aina ya siri ni muhimu katika kugundua hata faida za ukubwa wa sehemu za siri.
Cha ajabu.....!
Tanzania mpaka yajulikanayo hunekana kama siri , ingawa wenyenavyo hawafanyi siri kutuonyesha ukubwa wa maeneo wayazungushiayo uwigo kuficha siri.
Pamoja na ustaarabu wa binadamu wengi katika ya faragha kuyaacha faraghani, huhitaji kuvua mtu nguo kugundua walio wengi hawana kificha sehemu za siri au hata imeshindikana kuvaa chupi nzuri.
Cha kutisha ni kwamba , kwa mwendo huu walio wengi watafikia kubakia na siri moja ambayo sio siri ,kwa sababu tayari unaona MATAJIRI na WANASIASA  wanajijengea ngome ili wengi wasione  kifichwacho kwa siri.
Na......
Wanasiasa wako makini , kutuibia mpaka maini
Nasi kwa matumaini , twategemea matatizo yetu watakabili
Labda tuwakumbushe...
Kitu tusichokijua  kwa mtu tusiyemjua tunayepishananaye , chaweza kuwa ndio kilichotuhakikishia usalama au kukabwa hata pale sehemu tunapopajua.
Na inajulikana.....
Matajiri wanaogopa masikini na wanahitaji kujua SIRI ya  furaha   ya MPWEKE  apatayo kwa kuiangalia chupi yake yenye rangi nzuri  hata kama haitashuhudiwa na kipenzi katika kibanda cha faragha.
Na inajulikana .......
Wanasiasa wanajua kuwa sasa hivi  waliowengi wanastukia kuwa hawafaidiki na siasa zao ingawa  bado wanadanganyika kirahisi kwa stori za danganya toto ambazo zinakubalika kutokana na kitu ambacho sio siri chenye uhusiano na elimu na umasikini huohuo.
Muhimu kukumbuka kuwa , wenyenavyo hawataweza kufaidi walivyo kuwa navyo kama WASIONAVYO wataendelea kusahauliwa na kuendelea kutembea na siri ya machungu ya kukosa na kuwa na uhakika kuwa wenyenavyo ndio tatizo.
Wanasiasa na matajiri kumbukeni kuwa mtafaidi sana kwa kuhakikisha angalau na wengine wanapata mpatavyo hata kama vyenu  bado ni vya dhuluma.
Hakuna atakaye taka kukuvamia na kuhatarisha maisha yake ili akuibie TV yako ya inchi 120 kama angalau anako kaTV kake ka nchi 32.
Utafaidi kutembea na LIFERARRI lako ikiwa angalau na wengine wana vi  RAV 4.
Hata pesa za EPA labda hakuna ambaye angefuatilia sana kama watu wangekuwa wamejazwa mapesa angalau ya kuwa na uhakika familia itakuwa poa tu kesho na kesho kutwa, na hata vijipesa vya kuongezea maisha kutokana na kale ka UKIMWI, zipo.
Labda.......
Inategemea unaficha nini , kwa umahiri wako  wa chaguo la ukubwa wa sehemu  za siri  kuwa mahiri.
Kifichikacho leo , kucha yake yaweza kukiumbua kesho .
Ikiwa huna ili, labda lile au kile chaweza kukahidi kuingia kwa ulaini katika pango hilo la siri.
Ukubwa wa jambo la siri waweza kugundulika SIKU ya KUFA kwa NYANI ambapo miti yote huteleza.
Swali:
- Hivi umevaa chupi nzuri ee?
 
- Hivi unataka chupi yenye rangi nzuri kutokana na yule akusaidiaye kuivua atakavyokujaji kutokana na kificha faragha au pale uianikapo mbele ya macho ya jamii?
 - Hivi maswala ya chupi ni maswala ya faragha eeh?
 - Unauhakika ninaongelea upumbavu gani?
 
DUH!
Naacha topiki!
Ngoja tumpate Henri Salvador aje tena na Jardin d'hiver
Au tu HAFSA na BANANA ZORRO watupe kitu PRESSURE.
 



0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment