Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UnaUHAKIKA wa TAMUTAMU ya MKE au MME wako wa KWANZA kabla HUJAONJA, hujaoa au kuolewa na LIMTU la PILI au la SITA?

>> Monday, October 13, 2008

Inasemekana kula UGALI na MAHARAGE kila siku hukinaisha kama tu ukila PILAU au MABIRINGANYA kila siku.

Inasemekana kuwa baada ya kuchoka kula kiporo cha wali na maharage yalioungwa na nazi ya jana uyapendayo,vyakula vyote vitakavyofuatia vitakuwa vitamu na vitakusaidia unogewe tena na wali na maharage ya jana yalioungwa na nazi hapo siku za baadaye.

Lakini...
Ukiongelea chakula, labda ni tofauti na ukiongelea binadamu.
Inasemekana mapenzi ya binadamu na chakula , yanalemea upande mmoja, kutokana na chakula kutokuwa na kauli kuhusu jinsi gani kinafikiria ukilavyo au ujilambavyo.

Swali:

  • Katika mapenzi yako , umpendaye ana kauli zaidi ya kudai leo hajisikii vizuri kunanihii?
  • Unatumia kigezo gani kupenda chakula ambacho hutumii kulipenda LIMTU lako?
Utamu waKIMADA au LILE TU JAMAA ambalo JAMII , DINI au KAUBONGO KAKO kanakukataza KUONJA , kutokana na kukaaminisha KAUBONGO KAKO kuwa JAMII , DINI au KAUBONGO KAKO ni kautamu KALIKOKATAZWA, ni UTAMU tu ambao UBONGO wako unatafsiri kuwa ni tofauti kidogo na kautamu upatako kwa mke au mume wako.


Lakini.....

Si kweli kuwa LIKIMADA lako au LILE LIMTU lalo la nje ni tamu kuliko LIMTU lako LA NDANI.

Lakini......

Limtu la nje linaweza likasababisha unogewe zaidi na LIMTU lako la ndani, kama tu liwezavyo kufanya ukawa unalipa limtu lako la ndani mgongo ukilala na kudai kuwa umechoka wakati unalifikiria na kuliota limtu lako la nje.

Swali:
  • Sasa utajuaje UTAMU kama hakuna UCHUNGU?

Udhaifu wa binadamu ni pamoja na kuumia roho, wivu na ubongo kujifunza kitu baada ya kugusa moto. Ukigusa moto ukaungua , utataka kuufunza ubongo kukukumbusha usiguse tena moto. Ukionja tamu, utataka uufunze ubongo jinsi ya kupata tamu ili urudierudie kuonja tamu.

Cha kushangaza ni kwamba , ladha chungu unaweza kuufunza ubongo ukaona ni tamu. Ndio maana kuna wadaio kuwa walipoonja BIA mara ya kwanza waliona ni chungu ingawa leo wanadai ni tamutamu kunoga. Labda ndio maana afurahiaye MAZOEZI ukamwambia kuwa anachofanya ni ADHABU , atadai anaumia na haoni tamutamu ya mazoezi.



Swali:
  • Unafikiri Utamu ni nini?
  • Unafikiri WAKUBWA wazima wangapi wanaweza kuona maziwa ya MAMA ni MATAMU kama toto lilozaliwa tu na bila aibu linajua CHUCHU inatoa nini?

DUH!

Kama toto lilozaliwa tu linajua maziwa ya mama ni matamu, labda utamu hauhitaji kitu chakufananishia.

Lakini .....

Labda penzi la MUME na MKE linatakiwa liongezewe vikorombwezo kama tu toto linyonyalo liongezewavyo aina nyingine ya chakula jinsi siku zinavyoenda .

Lakini.......

Labda jinsi uongezeavyo vikorombwezo kwenye penzi lako na limtu lako ni sawa tu na jinsi toto uliongezeavyo milo mingine lifanikiwavyo kuongeza UJAZO wa MAVI na harufu ya kinyesi.


Lakini.......
Labda WEWE na Penzi lako na LIMTU lako ni tofauti na YULE na LIPENZI lake, na kama upendavyo kubadili vitumbua na kula maandazi siku mojamoja au tisatisa, ndivyo YULE aridhikavyo na UJI wa MIHOGO kila siku.


Lakini.......
Labda huwezi kabisa kufananisha mapenzi ya mtu na mtu na mapenzi ya mtu na chakula kama tu ushindwavyo kula mihogo huku ukilazimisha kaubongo kadhanie unakula keki.



Swali:
  • Unafikiri kuna kitu mtoto anafananisha dunia nacho kimfanyacho akizaliwa tu aanze kulia?
  • Si inasemekana ukiwa unajichua mwenyewe, kujirutubisha mwenyewe au hata unafanya penzi na usiyempenda, unaweza kujenga akilini picha ya umpendaye kama wafanyavyo baadhi ya MALAYA na siku moja moja unaweza kudakwa kwa kukosea jina la limtu lako kwa kutaja jina la kipenzi chako UKIPENDACHO kikweli MOYONI, AKILINI na ROHONI?

Sasaaa...

KUMBUKA nawaza tu HAPA , halafu Topiki imenishinda!:-(

Naacha basi!

  • Nakutakia kila la heri ambaye unajua utamu wa aina moja tu!
  • Nakutakia kila lakheri ambaye unajua tamutamu mbalimbali lakini tamu uliyonayo unaamini itakuwa inanoga hivyo hivyo kubwa kuliko kesho au hata kesho ya mwaka kesho.
  • Nakutakia kila la kheri ULIYEACHA tamu ya zamani ukidhani TAMU MPYA ni tamu kubwa kuliko na kugundua kuwa tamu ya zamani ndio ILIKUWA tamu HASWA na haipatikani kwa utamu ule tena.KIBEBA TAMU kimeshastukia HUNA MPANGO!:-(

YOTE MAISHA !
SI ndio UBINADAMU AU?
BAADAYE BASI!

Nakuacha na zilipendwa kutoka South AFRICA kutoka kwa CHICCO akikuambia WE CAN DANCE

Au ngojea tu Professor Jay akuambie HAPO SAWA.

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:57 am  

Kaka Simon asante kwa mawazo/mafundisho. mchana mwema

MARKUS MPANGALA 7:34 pm  

mmm utamu ni nini viele mnikumbushe? jamani hizi falsafa haswaaaa yaani ... lakiini kweli likimada na lile limupenzi mbona halinipi kama linavyofanya lile la kule kijijini ngoja nilikomoe niongeze lingine lakini kwa muda halafu nitakuwanalo lingine pale madongokuporomoka. mmm jamani mi haoi

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP