Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA kusoma BLOGU za PICHA na KUANGALIA blogu za MAANDISHI!

>> Friday, October 31, 2008

Inasemekana picha moja huzidi maneno elfu nakadhalika tatu na nusu!

Labda ni kweli picha moja hufikisha ujumbe kirahisi kuliko maandishi elfu ziro.

Haki ya nani tena!;huhitaji kujua Kichina ukiona picha, kustukia labda wanaongelea swala la taaluma ya jinsi ya kukojoa porini.

SWALI:

  • Si umeshaona picha ya Yesu ingawa unajua hakukuwa na kamera wakati Mtume Mohamedi anaoa?
Lakini......
Labda wakati wote mnaangalia picha moja , kuna apataye ujumbe wa matiti wakati wewe unaelimika kwa ujumbe wa matako.


Labda wewe unaona jalala na kuhisi pananuka uvundo, wakati mwenzio anastukia kuwa bado kwenu hamjaishiwa chakula.


Labda wewe unaona picha nzuri wakati yeye anahisi unakamera nzuri!

Labda blogu za picha zimepiga ngwala blogu za maandishi, kwa sababu ni rahisi kuangalia picha za MUNGU katika blogu za video.

Swali:
  • Ushawahi kuona picha ya MUNGU alivyopendeza?

  • Unauhakika na tafsiri za ujumbe wa picha?




Basi tumcheki jamaa akikojoa...
Photobucket
  • Unauhakika umeona eeH?
Au tuangalie tu picha za uume au uke
  • UMEONA eeh?
Pumzika kidogo basi tuangalie picha ya Mungu wa watu fulani pale Duniani ,karibu kidogo na pale mijusi wafanyiapo mapenzi.....
Photobucket
Labda picha , maandishi na hata sauti yako ingawa unanuka mdomo sasa hivi,vyote hufikisha ujumbe kuwa hakuna kinacho dumu.

Labda picha , maandishi na ukininongoneza, vyote vitabaini umebadilika , pamebadilika au cha moto utakiona kwa sababu ile kitu haiko pale tena.

Labda ujumbe uupatao kwa kirahisi kwenye picha kama ilivyo sababu yako yakutotaka kusoma maandishi ,hauna uzito wowote wa zaidi ya ujumbe:
PICHA hii NZURI!


Naacha basi Mkuu!
Topiki imenishinda!:-(
Ngojea MUTABARUKA aghani shairi DIS POEM

Au ngojea tu Maxi Priest afikishe ujumbe kwa mwanamke kuwa anataka tena, katika ONE MORE CHANCE

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 6:51 am  

mkuu hapo kwa nabii tu,
dis poem,ujumbe tosha kabisa.

Simon Kitururu 12:59 pm  

@Rasta:Si utani!

MARKUS MPANGALA 5:35 pm  

hii kali sana mkuu kwani naona kila mstari unapasua kichwa mpaka magogoni-ikulu pale

KKMie 5:36 pm  

Picha inawakilisha ujumbe tofauti kama nilikuelewa hapo ni kwamba kila mtu anaelewa kutoakana na anavyoiona picha hapati ujumbe uupatao wewe au mimi.

Inawezekana picha yako inaonyesha unakojoa na ndio ujumbe lakini mimi nikapata ujumbe kuwa uume ni mzuri au nywele zako zinang'aa au shati lako ni low material n.k.

Mimi zamani nilikuwa mvivu sana kusoma kwa vile sikuwa nikiandika, then nilipoanza kuandika ikanibidi wakati mwingine nisome ili kuwa na uhakika kama naeleweka ili msomaji aweze kuelewa.

Nikagundua kuwa ukisoma sana unakuza upeo wako na unaelewa zaidi na actually unaweza kutunza kumbukumbu na kumueleza mtu mwingine exactly ulivyo elewa tofauti na picha au hata Vid.

Napenda kazi yako Si. Kaza butizo.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP