Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UHAKIKA wa kununa KESHO!

>> Friday, June 27, 2008

Kesho yazaliwa leo
yakusubiri KESHO


Nyoka ujauzitoni
ajifunza panya KESHO kitoweo

Binadamu mitumbani
awezajua KESHO chupi yawezawasha

Tokea MTU leo azaliwe
tegemeo la KESHO

Anakula au kulala
ili nguvu zimsalani KESHO

Shuleni ajifunza ujinga
ili ikabilike KESHO

Apata mimba,
ili kumpa mimba TAIFA la KESHO

Njiwa sekundeni leo
Nani amuhakikishia ana KESHO?

Funzo ,
kesho uko hai.
Msuli upo kununa KESHO?

...........................XXXXX...................

Usitishike MDAU!
Nawaza tu ya KESHO, kwani sina uhakika na ya leo.

WEWE je?
Kila laKHERi kwa leo yako ili ikusaidie kesho yako iwe KULIA zaidi ya KUSHOTO!
HASA ikiwa fikira zako kuhusu kushoto ,ziko karibu na tafakari ya mchambia kono la shoto.

BASI Mkuu naacha topiki!

Tulia kidogo TAMANI KAONDO akukumbushe unaweza kuwa MPWEKE kesho.



AU kama MAJAZZ yanapanda, Mcheki kipenzi changu katika BASS na JAZZ kwa ujumla Mwanadada ESPERANZA SPALDING

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP