Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ni kweli MUDA HAUTOSHI!

>> Thursday, April 02, 2009

Lakini kama muangalifu unaweza UKAJISTAAJABISHA kwa kustukia ukubwa wa uwezayo kufanya ndani ya DAKIKA.

Ni kweli unaweza mpaka kupata mimba au kumpa mtu mimba ndani ya sekunde kama tu uwezavyo kufanikiwa kupata UKIMWI!

Na labda....
....... kama unataka ufe kwa furaha hasa kama unakumbuka kuwa ni lazima utakufa, basi jaribu KUFANYA YOTE uwezayo ili USIJILAUMU!

Labda:

  • Furahi zaidi ukiwa na chakufurahia!
  • Huzunika vya kutosha kwenye cha kuhuzunisha!
  • Saidia zaidi uwezapo kusaidia!
  • Kubali kusaidiwa ukishindwa!
  • Fanya UJINGA ukijua kuwa ni UJINGA!
  • Fanya ya BUSARA ikiwezekana!
  • Tukana!
  • Kubali kutukanwa wakati unafikiria maana ya tusi!
  • Fanya DHAMBI!
  • Tubu kama dhambi inakusuta!
  • nk.
Kumbuka,...
.... LABDA muda hautoshi ndio maana wakati unafanya hili HUFANYI LILE!


Labda ...
.... sio chaguo lako KUTOFANYA hili ingawa ni CHAGUO lako KUFANYA LILE!

Swali:
  • Unauhakika ni kwanini unafanya hili sasa hivi?
  • Unakumbuka kwa kutochukua hatua fulani ya kufanya KITU maana yake BADO UNASAIDIA kitu fulani KIFANYIKE?

Pamoja na yote ,...
... ni kweli MUDA HAUTOSHI!:-(


NIMEACHA wazo!

Tulia na MSONDO NGOMA MUSIC BAND katika kibao - Majuto


Au tu Papa Wemba aseme - Awa Yo Okeyi

Read more...

MPAKA MWEMBAMBA kati ya KUPOTEA katika YA MUHIMU na KUPOTELEA katika UMUHIMU!

YA MUHIMU na YASIYO MUHIMU hutenganishwa na mpaka ULIOKONDA.

Na,..
.... unaweza kupoteza UMUHIMU kwa KUPOTELEA katika YA MUHIMU.



Ni kweli,...
... mambo ya muhimu yanahitaji muda wako INGAWA unaweza kupoteza UWEZO WA KUSTUKIA umuhimu wa ya muhimu kwa KUBOBEA SANA kwenye ya muhimu mpaka UKAPOTEZA NI KWANINI MUHIMU!:-(


Kumbuka KUBALANSI umuhimu wa YA MUHIMU na YASIYO MUHIMU kama hutaki KUPOFUA jicho lako la maisha katika YA MUHIMU hasa hapa duniani PALIPOJAA yasiyo MUHIMU.


Kumbuka,...
....yasiyo muhimu ni MUHIMU kama unataka kutunza afya ya MUHIMU!

Na kukazania ya MUHIMU tu sio AFYA!

Swali:

  • Au?


Tulia na MLIMANI PARK ORCHESTRA kwa hisani ya tizedboy na kibao - MV MAPENZI

Au tu SAM MANGWANA amzungumzie -KABIBI

Read more...

KUHUSU BUSARA za asiyestukia BUSARA!

>> Wednesday, April 01, 2009

Katika kubalansi ujinga na BUSARA,....

......BUSARA ni busara kwa atafutaye BUSARA!

BUSARA haina tofauti na ujinga kwa asiyetafuta BUSARA!

Busara ni ujinga kama busara haieleweki kuwa BUSARA!

BUSARA!

Busara hataiwe ni ujinga BADO ni busara itambulikapo kuwa ni BUSARA!

____________------------------------_--------
Nawaza tu!
Swali:
  • Unauhakika gani busara ni busara?


Tulia tupate WISDOM of the BUDDHA....



Au turudi Tanzania kwa JHIKOMAN aseme - GULIGANDA

Read more...

WAKATI tunaishi KATIKA jamii ya WAOGOPAO kujulikana WANAONGEA UJINGA!

Kuongea ujinga hakupo PWEKE ingawa jamii ya WENYE BUSARA hujifanya KUMSHANGAA aongeaye UJINGA.

Tatizo ni kama ,....
... wafikiriao wanasoma au kusikiliza UJINGA hawafikiriii kwa nini wanafikiri wasomacho au KUSIKILIZA ni UJINGA.

Swali:

  • Ushawahi kufikiria ni vigezo gani vifanyavyo UJINGA ujulikane kuwa ni UJINGA?
  • Unauhakika uko huru kujulikana KUWA huwa unaongea UJINGA?

Nimeacha!

Tulia na Ochestra Super Mazembe katika - SHAURI YAKO

Read more...

NIVULIE CHUPI!:-(

KUNA sababu kwa nini SENTENSI ''NIVULIE SHATI'' haina mvuto kwa MTU FULANI kama sentensi ''NIVULIE CHUPI'' ingawa kwa KIISLAMU kitovu kikionekana nje au MAGOTI yakishuhudiwa bila kufichwa na BICHI KOMA, basi wewe OFISHALE uko UCHI!


NA,..
....KATIKA SIMULIZI za uvivu na kama jinsia inafaa kibandiko AU ombi LA;........NIVULIE CHUPI kuna uwezekano una CHUPI ndiomaana unataka kuhakikisha kama ni kweli naongelea CHUPI!:-(

Ngojea nijaribu kulalamika katika mistari HAFIFU ya...... kuangalia sentensi ''NIVULIE CHUPI!''

..................................................................................________________.....



VUA nione!
UKIVAA ni mwanzo wakuIchafua CHUPI KUBWA uliyoIvalisha matako madogo, ....
......UNAJUA?



CHAFUA tuone!
KUFICHA uchafu ni juhudi ya wajifanyao wasafi ,...
....wewe UNAJUA?



UKIMVULIA yeyote labda UNATAKA akuone!
LIPO hilo na labda unahitajika kujua ipo, ...
...UNAJUA?


USIPOJIVUA labda bado umevuliwa na huoni kabla hujavua uvuliwe UONE!
Lakini,...
.... UNAJUA?



WAKATI umevaa labda umevaa UONE!
UNAFIKIRI bado ukifunika,...
.... UTAJUA?

------------------------_______________----------------
Jaribu kusoma POINT of VIEW


NIMEACHA na ninawaza tu MHESHIMIWA usitishike usipoelewa My Point of VIEW!
SAMAHANI!

Swali:
  • AU?
  • Ushawahi kuomba maji au kuomba kuvuliwa hata SHATI katika dunia hii ikuogopeshayo kuomba kuulizia kushoto ni wapi ikiwa uko KUSHOTO?
  • Unauhakika uko KULIA?

Ngojea tupate mapenzi HAYA hasa YA katika kutokuwa naye leo usiku kwa msaada wa JUDY BOUCHER akinong'ona kuwa - CAN'T BE WITH U TONIGHT..

AU tuendelee kwa kwenda HAITI kukutana na T-VICE aseme -Pou Janm Pale..

Read more...

KWA JINA la PAPA MTAKATIFU BENEDICT wa XVI, usitumie KONDOMU!

Dini NI nzuri kwa sababu inatusaidia kutofikiria SANA katika DUNIA HII ihitajio KUFIKIRI KUBWA KULIKO kwa kutufariji kwa kutupatia WALE tuambiwao kuwa YAO ni KWELI na UKIAMINI ni KWELIKWELI. :-(

Unaweza kumbishia Mtakatifu SIMON KITURURU kwa sababu hujaambiwa au KUFUNDISHWA na umuaminiye kuwa SIMON KITURURU ni MTAKATIFU na anabikira ya TONGOTONGO.

Lakini labda,...
...kwa jina la Papa MTAKATIFU asiye wa Kikatoliki au wa KINZABANGA Simon KITURURU, katika dini yake ukiifuata anaweza akawa anasema ukweli wakitakatifu kuwa UKIPEKECHA,...

.....huwa inapata JOTO katika MPEKECHO.

Swali:
  • AU?
  • Kwa wakuulizao au kukushauri jinsi ya kutumia KONDOMU, unauhakika wanajua staili yako ya KUDINDA?
Jikumbushe What the Pope DO
  • Unauhakika naweza kukushauri jinsi ya kutumia jiko la kuni wakati sijui kukata kuni wala jiko la kuni?

SIKUBISHIII!:-(

Lakini,...
... kabla hujachapwa KIBAO kama RAIS MWINYI kwenye maulidi kwa kushauri watu wavae SOKSI,....
Swali:
  • UNAJUA sababu za ukiwa na GOVI unadaka MDUDU na kumehakikishwa kisayansi unadaka ZAIDI KULIKO ukila bila KIFUNIKA KITUNGUU? Kongoli CIRCUMCISION vs AIDS
  • Unauhakika matumizi ya kondomu ni yako kama hudindishi kidindacho kwa manufaa ya KIDINDACHO kuhifadhiwa kwa muda kwenye hifadhi-KIPENYO kama unadinda?

SIKUBISHI kama wewe nimsikilizaji wawasio tumia koroboi wakufundishao kutafuta MBU wako wapi na koroboi!:-(

JINYIME TU kumkojolea kama unauwezo wa kujikojolea!
DUH!

Swali:
  • AU?
  • Nani kakuambia kuwa kuna akojoaye wakati BADO hakuna ateteaye mharisho hata wa KIPINDUPINDU ufananao na maji ya mchelemchele kuwa ni mkojo kwa sababu za kufanana rangi na mkojo kwa sababu za ujasiri wake wa KUPITIA njia ya mkato ya nyuma??
NIMEACHA!
NAwaZA tu MKUU na samahani kama ninakukwaza wewe MSTAARABU ujuaye kuchagua yakuongea HADHARANI!:-(

Tutulie kwa kwenda SOUTH AFRICA kupata tena AFROPOP na NANA COYOTE..


Au twende tu Rwanda kwa MWANADADA nimzimiaye arudishe kiswahili katika bomba la wimbo ...sikilizia basi SOMI aongelee -INGELE

Read more...

TAALUMA ya KUJIZUIA kuchungulia!

Wakati umestukia tundu, ....

..... labda kunakilichoVUJA!:-(

UKIHISI wanafanya SIRI ya TOBO,...
.... unaweza TAKA KUWACHUNGULIA wenye tobo hata kama MBELE ya TUNDU kuna hata kishimo chenye SIRI YENYE TOBO ujuayo, INGAWA KWAO ni tundu wasiloridhika nalo ingawa hutambulika kwenye MACHO kwao kuwa ni TOBO.:-(
Na,...
... kuchungulia BADO ni kuangalia HATA KAMA ni kwa SIRI na unajificha kwa WAO unaowachungulia.


BAFUNI au CHOOONI hakuna siri kama SEBULENI hujawahi kustukia ndio UNAHITAJI kuchungulia kama ni muhimu NA ,....
........ huleta BARAKA za MCHUNGULIO kama wewe umestukia siri zifaazo kuchunguliwa HUCHUNGULIWA ila HUJASTUKIA siri ziko wazi na LABDA ,....
....ziko SEBULENI ingawa huchungulii bado kwa kufikiri sebuleni si PAKUMCHUNGULIA wakati anaoga bafuni!:-(

Swali:
  • AU?

Kumchungulia MTU ni yako SIRI ingawa waweza MPAKA kumstukia MUNGU pale YAKIBINADAMU ukichungulia.
Swali:
  • Au?

NIMEACHA!
NAWAZA TU KUMBUKA!:-(

Jikumbushe baadhi ya maana ya LOOK au Peep
Tutulie kwa kurudi TANZANIA kukutana na MATONYA aongelee kitu- TAXI BUBU

AU tu ALI KIBA aendelee kuongelea -NICHUM

Read more...

ANDAA sherehe ILI usisherehekee!

Mwandaaji wa SHEREHE hana starehe ya KUSHEREHEKEA sherehe.

Wakati WENGINE wanasherehekea SHEREHE, wewe muandaaji wa kitengo UNAKAZI ya KUHAKIKISHA waliokuja KUSHEREHEKEA wanasherehekea.:-(

Swali:

  • AU?
  • Unakumbuka kuwa kama WEWE ni MUANDAA sherehe , ukifurahia KWENYE SHEREHE haina maana unafurahia sherehe?

NIMEACHA!

Tutulie na wenye BUSARA tukianza na RICHIE SPICE katika -YOUTH dem COLD...

Au tu tena BURNING SPEAR auimbie UMATI mambo ya dini yake na Mungu wake katika -DRIVER...



Asanteni WADAU WOTE na baadhi yenu hawa!..



Photobucket




Photobucket


Photobucket


Photobucket





Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP