Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ni kweli MUDA HAUTOSHI!

>> Thursday, April 02, 2009

Lakini kama muangalifu unaweza UKAJISTAAJABISHA kwa kustukia ukubwa wa uwezayo kufanya ndani ya DAKIKA.

Ni kweli unaweza mpaka kupata mimba au kumpa mtu mimba ndani ya sekunde kama tu uwezavyo kufanikiwa kupata UKIMWI!

Na labda....
....... kama unataka ufe kwa furaha hasa kama unakumbuka kuwa ni lazima utakufa, basi jaribu KUFANYA YOTE uwezayo ili USIJILAUMU!

Labda:

  • Furahi zaidi ukiwa na chakufurahia!
  • Huzunika vya kutosha kwenye cha kuhuzunisha!
  • Saidia zaidi uwezapo kusaidia!
  • Kubali kusaidiwa ukishindwa!
  • Fanya UJINGA ukijua kuwa ni UJINGA!
  • Fanya ya BUSARA ikiwezekana!
  • Tukana!
  • Kubali kutukanwa wakati unafikiria maana ya tusi!
  • Fanya DHAMBI!
  • Tubu kama dhambi inakusuta!
  • nk.
Kumbuka,...
.... LABDA muda hautoshi ndio maana wakati unafanya hili HUFANYI LILE!


Labda ...
.... sio chaguo lako KUTOFANYA hili ingawa ni CHAGUO lako KUFANYA LILE!

Swali:
  • Unauhakika ni kwanini unafanya hili sasa hivi?
  • Unakumbuka kwa kutochukua hatua fulani ya kufanya KITU maana yake BADO UNASAIDIA kitu fulani KIFANYIKE?

Pamoja na yote ,...
... ni kweli MUDA HAUTOSHI!:-(


NIMEACHA wazo!

Tulia na MSONDO NGOMA MUSIC BAND katika kibao - Majuto


Au tu Papa Wemba aseme - Awa Yo Okeyi

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 8:19 am  

Habari Mkuu Simon,

Simon kule jumuta ni sawasawa na kiza kinene,kaka ni heri utuambie kila kitu kimekwama kuliko kusubiri hivi.

rasta hapa.

Anonymous 8:20 am  

Habari Mkuu Simon,

Simon kule jumuta ni sawasawa na kiza kinene,kaka ni heri utuambie kila kitu kimekwama kuliko kusubiri hivi.

rasta hapa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP