Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika KUMCHUNGULIA Mtanzania akijifunza KIINGEREZA!

>> Friday, April 24, 2009

Hii shughuli wee acha tu na kukariri imo!

Na hii shughuli bado BINGWA ni MTOTO.
Swali:

  • Ushawahi kumchungulia na sio kumuangalia MTANZANIA akijifunza Kingereza?
  • Wewe unashuka ung'eng'e?
  • Hivi Rais wa Ufaransa ni fala eeh kwa kuwa ung'eng'e haupandi?


Katika hii shughuli unaweza kujikuta unabana pua ikiwa yote ni katika miondoko yakujifunza UNG'ENG'E.


Na unaweza ukajikuta unaiga mapozi ya Padre Wakiitaliano asiyejua Kiingereza akiongea ,yote ikiwa katika kudhani ni miondoko ya lugha ya Ung'eng'e, hasa katika kudhani Wazungu wote wanashusha UNG'ENG'E.

Na kama ni mpenda miziki ya HIPHOP , hukawii kujikuta Dar-es-Salaam umevaa nguo za Winter , yote ni katika kudhani mapozi na azungumzavyo 50 Cent ni Kiingereza safi mpaka usikie eti ni akina OBAMA katika Wamarekani Weusi ndio waelewekao na kushusha lugha ipaswavyo na sio akina P. DIDDY.


Na wale wampendao Bob Marley , basi jasho litakutoka tukianza kuongea Kijamaika kwa lafudhi ya KIPARE au KIHAYA.

Hii shughuli wee acha tu!

Lakini kujifunza lugha yoyote mtiririko wa kujua ni uleule!

Na huwezi kupatia kabla hujakosea mara kenda zisizohesabika!

Swali:
  • Unakumbuka mapozi yako wakati unajifunza Kiswahili au kwa sababu umezaliwa Tanzania unadhani ulizaliwa unajua Kiswahili?
  • Kwani kujua lugha ni mpaka uwe na lafudhi ya lugha?


Na kumbuka kumcheki ajifunzaye lugha, kuna starehe zake na bado BINGWA ni MTOTO.

Kumbuka kama unajifunza kukosea imo ndani ya huu mchezo.
Na kama kuna akuchekaye, kumbuka inachekesha lakini maishani kuna ulivyomcheka mtu na hiyo sio siri ya kuacha kunoa NANIHII kama lengo ni kujua NANIHII hata kama unachekwa kwa kithembe.


Na kumbuka mwisho wa yote , lugha ni kwa ajili ya mawasiliano.

Na kama Wakatoliki wanamuelewa Papa, basi kama mtu akikuelewa ndani ya sentensi ''ze milk is standing'' huongelei maziwa ya kunywa bali titi lenye misuli ya nguvu na ncha kali iliyonuna , basi ujumbe umefika na matumizi ya lugha yameshamaliza kazi yake.

Swali :
  • AU?
  • Umestukia hata uongee kwa ufasaha gani kuna tutakaoshindwa kukuelewa unamaanisha nini?
  • Ni Watanzania wangapi unadhani wanajua Kiswahili fasaha ambacho ndicho Kiswahili?

Nimeacha!
Ni moja ya wazo tu na WIKIendi njeMA!

Narudi tena Nigeria kwa Majek Fashek aongee...


Au tu TMK Wanaume FAMILY wadai -DAR mpaka MORO


ASANTENI WADAU WOTE msionitenga!
Nakuacha na baadhi za Picha na Washikaji!
Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket


Photobucket







Photobucket


Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:55 pm  

Afadhali umeacha:-( hiyo ya Dar mpaka Moro kali!!

Yasinta Ngonyani 2:09 pm  

Oh nimerudi tena hizi picha haikuwepo wakati natoa maoni yangu ya hapo juu. Hizo bia hizo hata hatukaribishani naona hapo ni kweli hakuna kulala hata kama hujala Mmh Kazi kwelikweli:-(

Anonymous 8:55 am  

amani mkuu.

rasta hapa.

Yasinta Ngonyani 11:49 am  

Bwana wa mawazo upo wapi?:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP