Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Unachotumia nguvu sana kujihami KUKIKANA labda ndicho kinacho KUTAFSIRI, ndicho WEWE!

>> Wednesday, April 15, 2009

Nikawaida kukana wengine wakikuhusisha na usichohusika kitu!

Ingawa unaweza kuchelewa kukana kama kitu uhusishwacho nacho kinalipa kitu!:-(

Ukijihami na kukana , ....
......ni wewe umejihusisha na kitu!

Ukikanacho sana, .....
......LABDA ndio kinacho kuwakilisha na KUKUTAFSIRI.

Upendacho kikutambulishe sana , ....
.......LABDA hicho sio chako kitambulisho bali ni chako KIFICHA SIRI.


Na malaya sana, ...
....labda ndiye amshindaye PADRE na ajulikanaye MTAKATIFU kwa kujua staili za kwenda mbinguni zilizo SIRI.

Na padre wa kikatoliki asiyefanya sana,..
......labda ndio amshindaye malaya kwa staili za matumizi ya sehemu za siri!

Na shekhe na mlokole sana,..
.... labda kwa shetani wataenda kwa yao tusiyoyajua ya SIRI!

Swali:
  • Ukitaka ujulikane msomi sana , hakuna uwezekano unajaribu kufanya Ile -BADO HUJAELIMIKA iwe au kubakia siri?
  • Kwa kuhakikishia watu una roho nzuri sana, sio tu udhaifu na mapungufu ya roho ya kibinadamu wataka kuyafanya siri?

Ni moja ya wazo tu usitishike!

Ngojea nimuache Fally Ipupa alete kibao- Bakandja kama alivyokipiga Dar-es-Salaam


Au tupitie Haiti nimuachie tena Misty Jean azungumzie - Maladie D'amour

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:40 pm  

Simon:-(

Simon Kitururu 3:54 am  

@Yasinta: :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP