Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kuendelea kuchunguza USHUJAA wa SHUJAA!

>> Tuesday, April 07, 2009

Shujaa ni shujaa kwa sababu anafanya usichofanya ukitumia AKILI.


Na kumbuka,...
... mashujaa karibu wote HUKUMBUKWA kwa JAMBO MOJA TU la kishujaa LILILOSHUHUDIWA katika maisha haya ya binadamu yenye mambo mengi YASIYOSHUHUDIWA.

Na ni kweli,....
.... unahitaji jambo moja tu ili ukumbukwe kama SHUJAA au MJINGA.

Na tendo la kishujaa karibu mara zote hukaribiana na tendo la KIJINGA zaidi kuliko tendo la BUSARA ndio maana ukikosea kidogo tu, jitihada zako za kutaka kuleta ushujaa zinaweza kutafsiriwa kuwa ni UJINGA.

Swali

  • Unauhakika wewe sio shujaa na hatujashuhudia tu TENDO MOJA lako ambalo litakuoanisha wewe na neno SHUJAA?


Kumbuka tu ,....
... mjinga umjuaye kwa ujinga kwa kuwa umeshuhudia ujinga , kuna wamtambuaye kwa jina shujaa kwa kuwa WALISHUHUDIA wake USHUJAA!


NIMEACHA!
Tupumzike kwa kubadili hali ya hewa na kusikiliza ni kitabu gani hakiuziki Kenya wakati tukifikiria ya Tanzania...

Ngojea JAMES DANDU aongelee- MPENZI


Au tu REMMY ONGALA aulize- MIZIKI ASILI YAKE WAPI?

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Taratibu 9:00 am  

Masikini James Dandu mungu amweke mahali pema album zake nzuri sana haswa Sina makosa alibadilisha vizuri sana, Itabaki zilipendwa kama ile origino kweli kizuri hakikai daima.

Simon Kitururu 1:06 pm  

@Mzee wa Taratibu: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP