WANAOANDIKA wanaandika nini kifanyacho TUSIOPENDA KUSOMA tusome AU tuone MAANDISHI yanaleta nyege ya MSHAWASHA?
>> Wednesday, April 22, 2009
Kusoma nishai, ...
.... ghafla unaweza ukasoma kitu halafu ukajua na kustukia kumbe unadalili za MIMBA!
Halafu,..
....kulalamika ni bomba la faraja kwetu wote NA karibu kila MTU ni PROFESA :-(
Wakati unalalamika kuwa vijana wa siku hizi hawapendi kusoma , KUNAUWEZEKANO unachangia KUSABABISHA tupende kuangalia TV na labda PICHA ZA UTUPU mtandaoni kwa kuwa unatuandikia maandishi yasiyonyegelesha watu kujifunza HESABU.
Lakini,...
... watu wasiposoma inasaidia !
Na kama unanibishia waulize MAPAPA wa KIROMA wakukumbushe enzi zile za waumini kutojisomea wenyewe BIBLIA jinsi ilivyokuwa starehe kuwasimulia watu biblia inasema nini halafu mtazamo wako na TAFSIRI ZAKO unakuwa ndio kweli tupu na hakuna wakukubishia.
Samahani LAKINI PAPA WAKIROMA!
Nilisahau kuwa watu hata siku hizi hawasomi biblia wala korani (ingawa vipo gesti pembeni ya kitanda tukienda kupona), kitabu cha JUMA na ROSA wala KAMASUTRA, na kwa kukubishia HUTEGEMEA ZAIDI ni kwa mtazamo wa nani MWINGINE wanafuata TAFSIRI ZAKE na mtazamo wake katika kuelewa njia ya kwenda mbinguni au tu ile ya LIMBWATA kidume aitulize nyumbani.
Na Lakini UNAYEANDIKA labda usitishike!
Bado tupo tunaosoma na kuandika hata ujinga kwa hiyo MHESHIMIWA ukiandika uandikayo YA MAANA na YAHESHIMA labda tupo tutakao soma hata kwa nia ya KUJARIBU KUKUELEWA TU au kujiweka katika mkao wa kutaka KUKUTUKANA , kwa hiyo usiache kuandika KINGUNGE.
Swali:
- Au?
- Hivi nilikuwa naandika kuhusu nini vile?
NA nimeacha KINGUNGE mheshimiwa!
Kumbuka ni wazo tu hapa MAWAZONI!
BAADAYE!
Ngojea Basi ERYKAH BADU alete -FUNKY NASSAU
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment