Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi hamu ya kuwa kama WAZAZI WAKO hufifia?

>> Thursday, April 09, 2009

Wakati unataka kuwa kama WAZAZI wako LABDA ni kweli wazazi wako hawataki uwe kama wao!

Kunauwezekano kabisa wazazi wako wanataka uwe kama WAZAZI WAKO walivyotaka kuwa na ikashindikana .

Na ni kweli,...
.....ukizaliwa tu wazazi wako ndio wanakuwa kioo chako na kama wanaongea Kichina kunauwezekano utaongea KICHINA.

Swali:

  • Unauhakika kuwa wewe hujawahi kama bado sio Mkristo , Muislamu au Mpagani kutokana na wazaziwako kutoamini kuwa ubinadamu ni dini?

Lakini ,...
..... wewe sio WAZAZI wako!:-(

Wazazi wako wanaweza wakawa wamefanikiwa mpaka unaweza ukataka kuwa kama WAZAZI WAKO,.....

....Lakini...
.... wewe ni WEWE!:-(

Na unaweza ukawa ni miongoni mwa ambao hawakulelewa na wazazi wao wakibaolojia lakini kuna waliokuwa kiioo chako cha maisha hata kama ni cha jinsi ya kuwa ombaomba au jambazi,...
...na....
....hao ni wazazi kinamna kama katika kundi, ni hao unaweza kukiri walikuwa kama wazazi wako wakati unawaelezea WATU kuhusu hao ila unataka tujue hawakukuzaa.

Labda hamu ya kuwa kama wazazi wako ikififia ndio mwanzo wa KUWAKOSEA HESHIMA wazazi.

Kabla hujaacha kuheshimu wazazi kwa KUSHINDWA KUFIKIA KUSTAHILI , jaribu kupata jibu la kiswali KWANINI....
  • Kwa nini wameshindwa
  • Kwa nini wangefanikiwa
  • Kwa nini
  • Na kwanini unafikiri jibu la yote ni kutoWAHESHIMU.

Na bado binadamu pamoja na kuwa tofauti, jinsi wengine walivyo kunasaidia kutengeneza sisi tulivyo.

Mwingine akivaa JINSI anaweza akawa ndio sababu tunavaa KODRAI .

Mwingine akivaa KODRAI labda ndio sababu tunavaa KODRAI.

Hamu ya KUTOKUWA inaundugu na HAMU YA KUWA, na kwa hivyo anayetaka KUWA kama wazazi wake na ASIYETAKA wote wanafanya jambo moja ukizingatia kuwa hakuna mtoto aishiye katika umri na wakati sawa na WAZAZI wake . Nikiwa namaana wakati mtoto ana miaka mitano mwaka 2000 labda Mzazi alikuwa ana miaka hiyo mitano mwaka 1960 na hauwezi kulingana na wazazi wako ingawa mnaishi pamoja.


NAWEZA kusema,...
.....ukitaka kuwa kama wazazi au usipotaka kuwa kama wazazi vyote ni vitendo vya kujaribu tu lisilowezekana.
Swali:

  • Unauhakika kuwa unamjua hata mtu mmoja aliyefanikiwa kuwa kama wazazi wake?
NI MOJA ya wazo tu na sio kweli tupu!

Baadaye!

Ngojea Bozi Boziana anisaidie kubadili hali ya hewa kwa kibao-Demayo

Au Peter Tosh arudie kuongelea msiba katika -Burial

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP